Kiungo mkabaji wa Simba,Jonas Mkude amesema mechi dhidi ya Azam inahitaji akili zaidi.
Simba watakuwa wageni wa Azam, Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara.
"Azam
si timu ya kubeza walianza vema mechi yao na Ndanda kwa kuwafunga bao
1-0 na kujikusanyia pointi tatu na sisi tuliwafunga Ruvu Shooting kwa
mabao 7-0, kila mtu ana hamu ya kuona anaendeleza furaha,"alisema Mkude.
Alisema
anaamini Simba itaibuka na ushindi mnono dhidi ya Azam kwa madai
wamejipanga kuhakikisha wanaendeleza gurudumu la ushindi.
"Hakuna
kazi rahisi kwani kila timu ipo kwa ajili ya kuvuna pointi tatu ndivyo
ilivyo na kwetu kuona tunafika mbali na mwisho wetu uwe ubingwa,"alisema
Mkude
Post a Comment