Mkuu wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi mhe.Sarah Chiwamba akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa leo septemba 30 katika viwanja vya KKKT vilivyopo kata ya Nangando.
wananchi walioudhulia kwenye mkutano wa leo uliitishwa na mkuu wa wilaya ya liwale
wananchi walioudhulia kwenye mkutano wa leo uliitishwa na mkuu wa wilaya ya liwale
Mkuu wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi mhe.Sarah Chiwamba amewataka wakulima kuacha tabia ya kuuza korosho kwa walanguzi maarufu kangomba na awasitiza wakulima kufungua akaunti banki ili kuweza kulinda usalama wa fedha pamoja na uhai wao.
Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hazala na wananchi ulifanyika leo septemba 30 katika viwanja vya KKKT vilivyopo kata ya Nangando.
Mhe. Chiwamba amesema ameamua kuitisha mkutano na wananchi ili kuweza kujadili kwa pamoja masuala mbalimbali yanayohusu ufunguzi rasmi kwa msimu mpya wa korosho octoba mosi mwaka 2017/2018.
Mkuu wa wilaya amepiga marufuku ununuzi wa kangomba na kusema serikali umejipanga ili kuweza kukomesha biashara ya kangoma pia amewata wakulima kufungua akaunti banki ili kuweza kuondoa upotevu wa fedha kama uliotokea msimu uliopita na aliongeza kusema kuwa upo umuhimu mkubwa wa kufungua akaunti kwani ni njia salama ya fedha yao pamoja na kulinda uhai wa mkulima
”Msimu wa mwaka 2016 baadhi ya wakulima wasiofungua akaunti walikumbukana na changamoto nyingi sana ikiwemo wengine kuibiwa fedha zao pamoja na kupoteza maisha kutokana na kuvamiwa na watu na munatakiwa kuwa na nidhamu na matumizi ya fedha munayoipata ili iwe na tija na mukumbuke kuwekeza kwenye elimu ”alisema mkuu wa wilaya.
Kuhusiana na suala la kuchangia shilingi 30 kupitia zao la korosho katika mfuko wa elimu baadhi ya wakulima walikuwa na maoni tofauti wakisema kiasi hicho ni kikubwa na mzigo mkubwa kwa mkulima kwani serikali iliamua kufuta baadhi ya tozo ili kuweza kumkomboa mkulima.
Bwana Musa Mkoyage ni mkulima akizungumzia juu ya suala la uchangiaji huo wa mfuko wa elima alisema kuwa kiasi kilichopangwa ni kikuwa na kitakuwa mzigo kwa mkulima kwakuwa uchangia huo mfuko wa elimu umelengwaa kwa zao moja tu la korosho.
Katika hatua ingine baadhi ya wakulima kama Chande Kilubuniki na Saidi Kikalainde wameiomba serikali kulinda maslahi ya wakulima, kuweza kupitia upya takwimu za wakulima ili kuweza kupata idadi sahihi na kuwapatia pembejeo kwa wakati zinazotoshereza mahitaji.
Kwa upande wake afisa ushirika Severin Mganga alisema kuwa msimu wa jana ulikuwa na changamoto mbalimbali lakini mwaka huu wamejipanga upya kwani walibaini kasero moja wapo iliyofanya viongozi vya vyama kuongeza idadi ya kilo ni kuandika idadi ya kilo kwa talakimu bila kuandika kwa maneno hivyo msimu huu idadi ya kilo itaandikwa kwa talakimu pamoja na kwa maneno.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Liwale,Justin Monko alikitolea ufafanuzi wa pembejeo alisema kamati za vijiji vya pembejeo zimefanya kazi mzuri shida ilikuwa mgahao mdogo na mahitaji yalikuwa tani 1000.
Lakini mgahao walipata tani 793 lakini zilifika tani 751 na tani 42 hazikufika pia pembejeo hazikufika kwa wakati na mgahao huo ulitokana na mauzo wa msimu wa mwaka jana wa tani 70,600.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Liwale,mhe. Mohamedi Mtesa aliwaomba wakulima kuweza wakukubaliana na mawazo hayo ya uchangiaji wa mfuko wa elimu ili mwisho wa siku kuweza kutoa majibu ya matatizo na changamoto kwenye sekta ya elimu kwa wilaya ya Liwale.
Post a Comment