Kutokana na maendeleo ya kasi ya kitechnolojia karibia kila mtu sasa hivi anamiliki kifaa kinachoweza kufungua website kama vile simu, table, laptop na desktops. Internet imekuwa eneo kubwa zaidi la kupatia habari kuliko magazeti ya kawaida au redio. Kutokana na hali hii nimeandaa hii tutorial kuwasaidia wale ambao hawajui kabisa kutengeneza website ili wapate pa kuanzia.
Si lazima uwe umesoma programing au umeenda chuo ili uweze kutengeneza website, siku hizi kuna nyenzo rahisi ambazo zitakuwezesha kukamilisha tovuti yako kirahisi kabisa kwa kuanzia leo tutatumia tovuti ya blogger.com kutengeneza tovuti yetu ndogo.
Hakikisha una google account
Cha kwanza unatakiwa uwe na google account, njia rahisi ya kuipata ni kutengeneza email ya gmail, nenda http://gmail.com tengeneza email yako, kama tayari unayo email tuendelee mbele.
Pa kuanzia mwanzo
Kwanza kabisa nenda website ya blogger
Utalogin na account yako ya gmail, ukishaingia ndani kwa juu upande wa kushoto utaona neno new blog click hapo kuna box la kujaza litatokea kama hili
![[IMG]](https://i.imgur.com/7SSDXw6.png)
Tittle- hapa andika kwa kifupi kichwa cha habari cha website mfano taasisi ndogo
Address- hapa andika jina la website yako litakalotumiwa na watu mfano kitaasisi.blogspot.com
Template- Hapa chagua muonekano wa website yako, ila usijali sana sababu baadae unaweza kubadili
Ukimaliza kujaza bonyeza create blog, hongera sasa hivi na wewe unamiliki blog. Kuanzia hapa utaweza kuweka vitu kwenye blog yako na kuiweka unavyotaka wewe.
Maana za maneno utakayokutana nayo kwenye dashboard yako ya blog
Ukishamaliza kutengeneza upya blog/website yako utaona kuna maneno mengi yametokea upande wa kushoto kama vile new post, pages, comments, earning nk. Nitayaelezea hapa chini kila mtu ayaelewe
1.Overview
Kila siku ukiingia kutengeneza blog yako utakutana nayo, hii inaonesha dondoo muhimu za website yako kama vile takwimu za wanaoingia kwenye website yako, habari muhimu kwa watengeneza website nk. haina maana sana kwenye mlolongo wetu huu.
2. Pages and posts.
Hapa ndio pa muhimu zaidi kama mtengeneza website unatakiwa kujua jinsi ya kuandika post na pages maana utavitumia mara kwa mara.
Post-Hizi ni zile habari utakazokuwa unaziweka mara kwa mara, mfano kama ni website ya shule post zinaweza kuhusu mikutano ya wazazi, matokeo ya wanafunzi, michango ya kusaidia shule nk
Pages-Hapa utaandika vitu ambavyo havibadiliki mara kwa mara kama vile eneo shule ilipo, ilianzishwa lini, masomo shule inayofundisha nk
Namna ya kuandika pages na post ni moja ukibonyeza new post/page kutakuja muonekano kama huu
![[IMG]](https://i.imgur.com/M6I9K4L.png)
Kwa juu kulipoandikwa post title utaandika kichwa cha habari cha post yako mfano WANAFUNZI WAFAULU MITIHANI YAO KWA KISHINDO na chini kwenye box kubwa utaandika dhumuni la hio post. Ukimaliza utabonyeza publish ili hio post iweze kuonekana kwenye website yako. Muonekano wa kuandika ni kama wa JamiiForums hivyo kuweka picha au kubadili maneno rangi havitakushinda
Kwenye page pia utarudia kama post ila vichwa vya habari vya pages vinakuwa vifupi mfano about us, location, home, customers nk
3.Comments
Utakapokuwa unapost vitu watu watakuwa na uwezo wa kuchangia maoni au pongezi kwenye habari ulioandika, kupitia sehemu hii utaweza kuziangalia hizo comments na kuruhusu unazoona zinafaa na kufuta unazoona hazifai
4.Google+
Huu ni mtandao wa kijamii kama facebook vile, hapa unaweza ukachagua kila unapopost kitu uwe unakishare kwenye google+, kama hutaki unaweza ukaeka off chaguo hili.
5.Stats
Inakaribia kufanana na overview utaona dondoo muhimu za website yako hapa
6.Earnings
Website yako ikiwa maarufu unaweza kujiingizia kipato, ila hili sio la kufikiria kwanza
7.Campaigns
Kama unataka kutangaza website yako hapa panakuhusu, ila hawatangazi bure watakutoza hela, hapa pia si pa kuangalia sana mwanzo
8.Layout
Lapa utapangilia muonekano wa website yako, kuna mambo mengi unaweza kufanya ila nitaelezea jinsi ya kufanya pages zako zionekane. Juu tumeelezea jinsi ya kutengeneza pages lakini zinaweza zisionekane hadi wewe mwenyewe upangilie zionekane vipi. kikawaida pages zinakaa chini ya header angalia hii picha
![[IMG]](https://i.imgur.com/OrnoloN.png)
Hio rangi kama damu ya mzee na neno taasisi ndogo ndio header na hayo maneno home, location na about us ndio pages zetu.
Jinsi ya kuweka page utaclick kwenye hio layout halafu tafuta sehemu imeadikwa cross column halafu click add/edit kutafunguka page ndogo click pages kutatokea kitu kama hiki
![[IMG]](https://i.imgur.com/x5SeC2Z.png)
tick page zako unazotaka zitokee halafu save.
9.Templates
Hapa ndio mahali unapoweza kubadili muonekano wa website yako kuna template hizo unazoziona na kuna nyengine unaweza kudownload na kuzieka. Nitapaongelea zaidi hapo chini
10.Settings
Hapa unaweza kubadili mambo mbali mbali kama jina la website, kuweka jina la .com, lugha nk
Mpaka hapa kama umefuatilia kwa makini utakuwa umeweza kutengeneza blog yako ndogo, unaweza kujiendeleza mwenyewe na kuiweka website yako kadri unavyotaka.
Jinsi ya kubadilisha template ya website
Kuna maelfu ya template za blogger kwenye internet hapa nitakuonesha jinsi ya kuzipata hizo template na kuzieka kwenye website yako.
Mfano search google maneno haya EDUCATION BLOGGER TEMPLATES
Result zikija chagua unayopenda halafu download template yako
Yangu niliotumia hii hapa EducationWeb Blogger template - BTemplates
Ukishadownload extract hilo file kwenye computer utaona ndani kuna file linaishiwa na .xml, rudi kwenye blog unapoeditia kwa juu utaona neno limeandikwa backup and restore kutakuja box la ku upload, uta upload themes yako na itaonekana kwenye website.
Kama umefuatilia mwanzo hadi mwisho vizuri utapata kitu kama hiki
Nafikiri leo umetumia muda wako vizuri kujifunza endelea kutembelea LIWALE BLOG
Post a Comment