0
Mahakama Kuu Kenya imebatilisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika August 8, 2017 ambao ulimpa ushindi Uhuru Kenyatta dhidi ya Raila Odinga na kutaka kuandaliwa uchaguzi mwingine ndani ya siku 60.
Mahakama hiyo imeeleza kuwa IEBC haikuandaa uchaguzi huru na wa haki ambapo Jaji Mkuu David Maraga ameagiza uchaguzi haukuandaliwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria, hivyo matokeo yake ni batili.
“Natangaza hapa kwamba Kenyatta hakuchaguliwa na kutangazwa kwa njia inayofaa. Agizo linatolewa, kuagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa na kufanyisha Uchaguzi mwingine kwa kufuata Katiba na Sheria katika kipindi cha siku 60.” – Jaji Maraga

Post a Comment

 
Top