Mfanyabiashara Yusuf Manji leo August 18, 2017 ameshindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya uhujumu uchumi kwa sababu za kiafya.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wakati shauri lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa ambapo alidai kuwa amepata taarifa kutoka kwa Askari Magereza kwamba Manji anaumwa na amepewa (AD) ya siku mbili.
Licha ya Yusuf Manji kutofika Mahakamani kwa sababu za kiafya, washtakiwa wenzake Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere walifika ambapo baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi August 25, 2017.
Post a Comment