Watoto zaidi ya 60 wamefariki dunia katika hospitali ya umma kaskazini mwa India, maafisa wamesema, huku kukiwa na tuhuma kwamba huduma ya gesi ya oksijeni hospitalini ilikatwa kutokana na deni.
Maafisa katika jimbo la Uttar Pradesh wamekiri kwamba hakukuwa na oksijeni katika hospitali hiyo lakini wakasema vifo hivyo havikutokana na hilo.
Kulitokea wasiwasi katika hospitali hiyo, huku jamaa wakijaribu kuwasaidia wahudumu hsopitalini kutumia mifuko ya gesi kuwasiadia wagonjwa kupumua.
Wengi wa waliofariki walikuwa katika kitengo cha watoto wachanga au walikuwa wanatibiwa ugonjwa wa encephalitis.
- Njiwa akamatwa na polisi India
- India yaweka rekodi ya kurusha satelaiti
- Likizo ya uzazi India ni miezi 6 !
Vifo hivyo vilitokea katika kipindi cha siku tano kuanzia JUmatatu katika hospitali ya Baba Raghav Das, katika wilaya ya Gorakhpur.
Watoto 30 walifariki Alhamisi na Ijumaa, hospitali hiyo imesema.
Afisa wa afya wa wilaya Anil Kumar amekiri kwamba kulikuwa na "suala kuhusu malipo" kati ya hospitali hiyo na kampuni inayowasambazia oksijeni, lakini akasema huenda vifo hivyo vilisababisha na mambo mengine kwani wagonjwa wengi waliolazwa humo walikuwa katika hali baya.
Eneo hilo ni moja ya maeneo maskini zaidi India na hushuhudia vifo vingi vya watoto kila mwaka kutokana na maradhi ya aina nyingi, baadi kutokana na encephalitis.
Kumar alisema watapokea mitundi zaidi ya gesi wakati wowote kuanzia sasa, na pia kwamba wamelipa deni.
.
Post a Comment