0

NA FATUMA MUNA

Diwani wa Kata ya Nyakahanga wilayani Ngara, Charles Bechumila ameshambuliwa kwa kuchomwa mishale ikiwa ni pamoja na kukatwa na panga na watu wasiofahamika alipokuwa kwenye ziara.

Kiongozi huyo anadaiwa alishambuliwa na watu wasiojulikana mapema leo alipokuwa kwenye msafara wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mhe. Godfrey Mheluka uliokuwa katika operesheni ya kuwaondoa watu wanaodaiwa kuvamia maeneo ya wafugaji katika Kijiji cha Kashanda.

Katika shambulizi hilo lililotokea leo Agosti 29 asubuhi, diwani wa Nyakahanga, Charles Bechumila amejeruhiwa na amepelekwa katika Hospitali Teule ya Nyakahanga.

Ofisa Tarafa ya Bugene Nyaishozi, Rozaria Christian amesema walikuwa kwenye operesheni halali na wakulima hawakuwa na  taarifa hivyo baada ya kuwakamata wawili ndipo kundi la watu lilijitokeza likionyesha kuwa lilijiandaa kuwashambulia.

Aidha Christian amefafanua kwamba watu kadhaa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika kumjeruhi diwani huyo na Mkuu wa wilaya hiyo, Mheluka amesema bado hayupo sawa kuzungumzia tukio hilo.

Post a Comment

 
Top