0
Mchezaji wa timu ya Vijuso fc akiwa anamiliki mpira kwenye mchezo dhidi ya Mitumba fc kwenye  hatua ya nusu fainali ligi ya Kazumari cup uliochezwa agosti 21 katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Michuano ya ligi ya Kazumari cup hatua nusu fainali jana agosti 21 kulikuwa na mchezo mmoja kati ya Mitumba fc dhidi ya Vijuso fc na matokeo mpaka dakika 90 ziliweza kutoana jasho la sare ya goli 1-1 mchezo uliopigwa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani.

Timu ya Mitumba fc ilikuwa ya kwanza kuandika bao namo dakika ya 42 lililofungwa na Faraja Hasani huku goli la kusawazisha la Vijuso fc likifungwa na Yuba Mmocha katika dakika ya 62.


Baada ya kukamilika kwa mchezo huo na matokeo kuwa sare ikafuata hatua ya mikwaju ya penaiti timu ya Mitumba fc ilipata mikwaju ya penaiti 4 na vijuso fc ilipata penaiti 3 na mlinda mlango wa mitumba fc akidaka mkwaju wa penaiti 1 kwa matokeo haya Mitumba fc kusubiri mchezo wa fainali dhidi ya mshindi wa leo agosti 22.

Leo agosti 22 kutakuwa na mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ambapo timu ya Mifugo fc itashuka dimbani dhidi ya Wachukuzi fc mchezo unaotarajiwa kuwa mkali kutona na timu  zote kuwa kivutio cha watazamaji wa soka kwani timu ya  Wachukuzi fc ndio timu mpya na imeaza vema mpaka kufikia hatua ya nusu fainali.

ANGALIA VIDEO YA MPAMBANO WA NUSU FAINALI KATI YA MITUMBA FC Vs VIJUSO FC

Post a Comment

 
Top