0

Muhtasari

  1. IEBC inatarajia kupokea fomu zote za matokeo kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana.
  2. Upinzani umedai Raila Odinga alishinda uchaguzi na kuitaka tume imtangaze kuwa mshindi wa urais
  3. Matokeo ya awali yanaonesha Bw Kenyatta anaongoza akiwa na kura 8 163 572 naye Bw Odinga ana kura 6 747 099.
  4. Matokeo ya awali ambayo yamepokelewa ni kutoka asilimia 99.04 ya vituo.
  5. Kura zilizoharibika zimeendelea kuwa nyingi, na kufikia sasa ni kura 399 935.

Habari za moja kwa moja

Kenyatta aendelea kuongoza matokeo ya awali

Matokeo ya awali yanaonesha Bw Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee anaongoza akiwa na kura 8 163 572 naye Bw Raila Odinga wa chama cha ODM kilicho katika muungano wa National Super Alliance ana kura 6 747 099.
Matokeo yaliyotangazwa ni ya vituo 40489 kati ya vituo 40883.
Kura zilizoharibika zimeendelea kuwa nyingi, na kufikia sasa ni kura 399 935.

Hujambo!

Karibu kwa siku nyingine ya taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika Jumanne. Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kenya (IEBC) inatarajia kupokea fomu zote za matokeo kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana. Tangazo la mshindi wa urais linatarajiwa kutolewa baada ya tume hiyo kuhakiki fomu hizo. BOFYA   >>hapa  KUANGALIA MOJA KWA MOJA 

Post a Comment

 
Top