Mchezaji wa timu ya Mifugo fc kushoto
akiuhai mpira kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Mitumba fc mchezo uliopigwa
agosti 25 katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.(Picha na Liwale Blog)
TIMU ya Mifugo FC imetawazwa kuwa mabingwa
wapya wa Ligi ya Kazumari cup 2017 baada ya kuitembezea
kichapo cha mikwaju ya penait mabao 5-4 dhidi ya Mitumba FC kwenye Uwanja wa
Halmashauri ya wilaya Liwale mkoani Lindi.
Mchezo huo uliochezwa agosti 25 nwaka 2017
ulianza kwa kasi kwa kila timu ilionekana kuwa na shauku ya kupata Bao.
Lakini timu zote zilionekana kupania
mchezo huo na ilianza kupata Bao la kuongoza kupitia kwa Yasini Nganyaga dakika
ya 40 na lidumu hadi mapumziko. Katika kipindi cha mchezo huo uliendelea kuchezwa
kwa kasi kwa kila timu ikisaka magoli lakini hakuna timu iliyoweza kuvumania
lango la mwezake mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili mpira ulianza
mchakamchaka kwa kila timu kutaka kuongeza goli lakini juhudi hazikuzaa
matunda na mchezo ulimalizika mpaka dakika zote 90 ikiwa sare ya 0-0.
Baada ya kumalizika mchezo huo dakika 90
hazikufungwana ilazimika kupigwa mikwaju ya penaiti katika hatuo hiyo ya
mikwaju ya penaiti timu ya Mifugo iliweza kupiga mikwaju ya penaiti 6 na kukosa
mmoja na Mitumba fc ilipiga mikwaju 6 na iliweza kupoteza penaiti 2 hivyo
Mifugo fc iliweza kupata penaiti 5 na Mitumba fc kupata penaiti 4.
Wakizungumza na mwandishi wetu Nahodha wa
Mitumba fc, Haikosi Mpwate alisema mchezo ulikuwa mgumu toka dakika za mwanzo
Lakini alikiri ugumu wa mashindano hayo na aliwashukuru wadau wa soka kwa
kuwasapoti na anashukuru kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo ya
Kazumari cup. Kwa upande wa Nahodha wa Mifugo fc, Karimu Libena alisema mchezo
huo ulikuwa mgumu kwa upande zote makosa yaliofanywa na Mitumba fc nao
walishindwa kutumia vema.
Na mdhamini wa ligi hiyo ambao ni Zalafi
Kazumari alisema ligi hiyo ilkuwa na lengo kuu ni kuwahamasisha vijana
kishiriki michezo kama moja ya ajira katika wilaya ya Liwale na aliongeza
kusema ligi litakuwa endelevu kila mwaka.
Zawadi za mtu mmoja mmoja kama
mshangiliaji bora alizawadiwa simi ya mkononi.
Mabingwa hao, wamejinyakulia fedha
shilingi. 800,000 wakati mshindi wa pili, Mitumba fc wakipewa zawadi ya fedha
shilingi. 400,000. Mshindi wa tatu ambao ni Vijuso fc walipata kitita cha
shilingi.200,000.
Ligi hiyo ilianza julai 22 mwa huu na ilishirikisha
jumla ya timu 11 ikiwemo timu ya Mifugo fc,Mitumba fc,Sido fc,Vijuso
fc,Wachukuzi fc,Storaway fc,Nyela fc,Mbaya city,New generation,Likongowele fc
na Market fc.
Post a Comment