Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuhakikishia Rais wa Uganda,Yoweri Museveni kuweka mradi wa bomba la kupitisha gesi kutoka Mtwara kwenda Uganda, baada ya ujenzi wa bomba kukamilika.
Rais Magufuli ameyazungumza hayo wakati akihutubia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa kusafirisha mafuta kutoka Hoima – Uganda hadi bandari ya Tanga.
“Kwa hiyo kuweka bomba ambalo litapitisha gesi wakati hili lingine linapitisha mafuta, inashindikana nini? Napenda kumuhakikishia muheshimiwa haya yanawezakana, bomba la gesi lipite hapa kwenda Uganda, Kama wao wametukubalia kwa nini sisi tushindwe, huu ndio ushirikiano wa Afrika Mashariki. Tuwapelekee gesi wakafufue viwanda vyao vya chuma kule”, alisema Rais Magufuli.
Hata hivyo kuridhia kwa Rais Magufuli kumekuja mara baada ya ombi la Uganda kupelekewa gesi lilitolewa na Rais wa Uganda Mh. Yoweri Museveni alipokuwa akizungumza na Watanzania
Post a Comment