0
Kutokana na kuwepo kwa vitendo vya wizi na uporaji wa mali za abiria katika vituo vya daladala vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojulikana kwa jina la wapiga debe ,Jeshi la Polisi kanda Dar es salaam limepiga marufuku shughuli za upiga debe

Jeshi la Polisi limeahidi kuwachukulia hatua baadhi ya madereva na makondakta watakao ruhusu magari yao kupigiwa debe na vijana hao

Kaimu kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lucas Mkonya amesema wananchi wengi wamekua wakipeleka malalamiko juu ya wizi huo unaotokea kwenye vituo vya daladala unaofanywa na baadhi ya wapiga debe kwenye vituo hivyo ambapo amesema jeshi hilo litaendesha oparesheni maalum katika vituo vyote vya daladala siku ya Jumatatu kwaajili ya kuwaondosha wapiga debe.

Suala la uwepo wa matukio ya uporaji wa mikoba pamoja na mabegi ya wakina mama na baadhi ya wageni kutoka mataifa mengine katika maeneo ya mijini ikiwemo Posta, Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewakamata watu ishirini na tatu wakiwemo vinara wanne wa matukio hayo ya uporaji kwa kutumia boda boda.

Aidha Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam katika oparesheni zake limefanikiwa kuwakamata zaidi ya watu 270 wanaotuhumiwa kujihusisha na makosa mbalimbali ya hihalifu ikiwemo unyang'anyi kwa kutumia nguvu na silaha na kukutwa na dawa za kulevya.

Post a Comment

 
Top