Je wajua kwamba mbu huvutiwa na vitu vitamu?.
Hivyobasi wanasayansi wametumia fursa hiyo kutengeza dawa iliochanganywa na sukari ili kuwavutia kwa lengo la kuwaua.
Dawa hiyo imechanganywa na kemikali iliowekwa harufu ya sukari inayoweza kuwavutia wadudu hao .
Imegunduliwa kuweza kuangamiza mbu katika vijiji vya Tanzania vyenye ugonjwa mwingi wa malaria ambapo majaribio yamefanywa.
Dawa hiyo kwa jina Vectrax inaweza kupiga jeki juhudi za kupunguza malaria, Zika na magonjwa mengine yanayosababishwa na mbu duniani.
Mwanasayansi wa Brazil aliyenzisha dawa hiyo Agenor Mafra Neto anasema kuwa lengo lake ni kuifanya kuwa ya bei rahisi na kuhakikisha kuwa imesambazwa kupitia Umoja wa Mataifa na mashirika yasiokuwa ya kiserikali.
"Mchanganyiko wa kemikali tunayotumia kuwavutia mbu una nguvu mno hatua ambayo inawafanya kutovutiwa na harufu nyengine za mimea ya kawaida'', alisema Agenor.
Anasema kuwa ni sawa na kuwa na duka la chocolate katika kila pembe.
Bidhaa hiyo ni kivutio kikubwa hatua inayowafanya kuila licha ya kuwa na kemikali za dawa ya wadudu.
Mbali na hilo mabaki ya dawa hiyo yanaweza kuchafua udongo na kuukinga dhidi ya wadudu.
Kwa kutengeza dawa hiyo wanasayansi hao walitumia harufu ya maua na mimea mingine inayotoa nekta .
Baadaye walitumia gesi ya chromatography-electroantennographic (GC-EAD) kutenga na kubaini vitu vyenye harufu mbaya ndani yake.
Waliweka antena za wadudu hao katika maelfu ya vitu hivyo kubaini ni vipi vinaweza kuwa na athari ya kibaiolojia.
Waliondoa harufu zozote ambazo zinaweza kuwavutia nyuki.
Baadaye walitumia mchanganyinko wa kemikali wenye sukari na protini kuigiza kemikali 20 zinazoweza kuwavutia mbu katika maua yanayotoa nekta na kuwashawishi kula.
Mchanganyiko maalum wa kemikali hizo na dawa ya wadudu kama vile pyrethroids ama spinosad ulitengeza dawa yenye nguvu.
Watafiti hao kwa sasa wanafanya utafiti nchini Tanzania ,ambapo asilimia 93 ya raia wako hatarini kuambukizwa magonjwa ya malaria.
Katika matokeo yao walibaini kwamba idadi ya mbu ilipungua kwa thuluthi mbili katika muda wa wiki mbili miongoni mwa jamii zilizotibiwa na Vetrax ikilinganishwa na zile ambazo hazikutibiwa na dawa hiyo.
''Iwapo hali itaendelea ilivyo, tunataraji kwamba idadi ya mbu wanaosambaza malaria itaangamia kabisa katika maeneo ya vijiji vilivyotibiwa'', alisema Mafra-Neto.
Ana matumaini ya kuwa na data zaidi kutokana na utafiti huo hivi karibuni.
Huku Mafra Neto akitambua kwamba mbu huwa na jukumu dogo katika chakula kupitia kuwasaidia wanyama wadogo kama vile samaki na buibui, angependelea kuwaona wachache hususan katika mataifa yalio na ugonjwa wa malaria.
Post a Comment