0
Waziri mkuu mheshimiwa Kassimu Majaliwa 
 Mbunge wa jimbo la Liwale,Mheshimiwa Zuberi Kuchauka 
 wananchi wakifuatilia kwa ukaribu hutuba ya waziri mkuu Kassim Majaliwa 
  wananchi wakifuatilia kwa ukaribu hutuba ya waziri mkuu Kassim Majaliwa 





  wananchi wakifuatilia kwa ukaribu hutuba ya waziri mkuu Kassim Majaliwa 
 Viongozi mbalimbali walioudhulia kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya kusikiliza hutuba ya waziri mkuu Kassim Majaliwa alipohutuba wananchi wa Liwale

   wananchi wakifuatilia kwa ukaribu hutuba ya waziri mkuu Kassim Majaliwa 


   wananchi wakifuatilia kwa ukaribu hutuba ya waziri mkuu Kassim Majaliwa 

  wananchi wakifuatilia kwa ukaribu hutuba ya waziri mkuu Kassim Majaliwa (Picha na Liwale Blog)


 Waziri mkuu mheshimiwa Kassimu Majaliwa ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Lindi, leo julai 10 amefanya ziara katika wilaya ya Liwale mkaoni Lindi kukagua miradi mbalimbalimba iliyopo wilayani hapa.

Waziri mkuu aliwahutubia mamia ya wananchi wa Liwale waliojitokeza kwa wingi  katika uwanja wa halmashauri ya wilaya huku akiwahakikishia wananchi kupata huduma za kiserikali kutoka kwa watumishi bila kujali uchana na amewaonya watumishi ambao hawatakuwa tayari kuwatumikia wananchi wajiondoe ili kuwapisha watumishi watakaoendana na serikali ya Rais John Magufuli.

Awali, Waziri Mkuu alizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale katika Ukumbi wa Tengeneza, ambapo amewataka Watumishi wa Umma Nchini kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa Wananchi. Amesema Watumishi wanawajibu wa kuwahudumia Wananchi bila ya kutengeneza mazingira ya kuomba rushwa na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri mkuu amehakikishia wananchi serikali ya awamu ya tano itaboresha miundombinu ya barabara ya wilaya ya Liwale ambazo zinazounganisha  wilaya za Nachingwea,Liwale na Nangurukuru huku barabara ya Liwale mpaka  Mahenge mkoani Morogoro imeweza kuondolewa kutoka ngazi ya wilaya na kuhamishiwa ngazi ya mkoa ili iweze kutambuliwa rasmi na kuweza kujengwa kwa kiwango cha rami.

Waziri mkuu Kassimu Majaliwa amesema serikali imefanya hatua ya awali ya kuwaleta wataalumu wa barabara kukagua barabara ya Liwale mpaka Nangurukuru kwa kuangalia sehemu za ambazo zitahitajika kujengwa madaraja na kuangalia kifusi kinachofa.

Pia waziri mkuu amewaagiza maafisa ushirika kuwaondoa viongozi wapya wa vyama vya ushirika waliochaguliwa upya ambao awali walibainika kuwahujumu wakulima  fedha zao  na hakuna kiongozi aliobainika kuwaibia wakulima kugombea uongozi wa ushirika.

“Serikali haitalipa fedha kwa wakulima bali viongozi waliokula fedha za wakulima adhabu yao ya kwanza ni kulipa fedha kwa wakulima na ninamwagiza mkuu wa wilaya kuwakamata viongozi wote waliokula fedha za wakulima” alisema waziri mkuu

Aliongeza kusema hivi sasa zao la ufuta wakulima bado wanaibiwa kutokana na zao hilo halina boda hivyo serikali imemtaka waziri wa kilimo kuliondoa zao la ufuta kwenye bodi ya mazao mchanganyiko na kuliweka kwenye bodi ya stakabadhi ghalani ili kuweza kuleta tija kwa wakulima wa zao la ufuta.

Wananchi wamehakikishiwa kupata kuhuduma bora za afya katika vituo mbalimbali vya afya vilivyopo wilayani hapa na serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya vituo vya afya kama kituo cha afya cha Kibutuka kujengewa kuchumba cha upasuaji huku akiipongeza halmashauri kwa hatua ya awali ya kutenga eneo hekari 50 la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.


Awali mbunge wa jimbo la Liwale,mhe. Zuberi Kuchauka aliongozana na waziri mkuu kukagua miradi mbalimbali iliyopo jimboni kwake huku akitumaini ujio wa waziri mkuu utaweza kutatua kero za wanaliwale huku akimwomba waziri msaada wa pembejeo haukidhi mahitaji ya wakulima kwani mahitaji ya wakulima ni mara tatu zaidi.

ANGALIA VIDEO WAZIRI MKUU AKIWAHUTUBIA MAMIA YA WANANCHI WA WILAYA YA LIWALE

Post a Comment

 
Top