0

 Wanafunzi  wa  shule  ya  msingi chumo  wilayani  kilwa 

 NA  SAUTI YA KUSINI. BLOG 

Baadhi ya wazazi na walezi  wilayani  Kilwa mkoani Lindi wamegoma kuchangia michango mbalimbali ya  maendeleo ya shule ikiwemo chakula za  wanafunzi kwa madai ya  kuwa  huduma  hizo  ni miongoni  mwa  zile  zinazotakiwa  kutolewa  bure serikali. 

Haya  yameelezwa  na wanafunzi,pamoja na  wajumbe  wa  kamati ya  shule  ya  msingi  Lihimalyao kwenye  kikao  cha kujadili changamaoto  za  elimu kilichoitishwa  na  shirika  la  Action  Aid na mtandao  wa mashirika  yasiyokuwa  ya  kiserikali wilayani  Kilwa (KINGONET).

Akizungumza  kwa  niaba  ya  wanafunzi  wa  shule  Lihimalyao  Selfu Mohamedi  alisema wazazi  wamekataa  kuchangia  chakula  kwa  ajili ya  uji kwa  madai huduma  hiyo  inatolewa  bure na serikali.
Selfu alisema sambamba  na  kukataa  kuchangia  chakula  lakini  pia wazazi  hao  hawashiriki shughuli zozote  za maendeleo  ya  shule kwani ikitokea   kazi  ya  ukarabati  wa  jengo au  ujenzi  wa  vyoo hawashiriki kabisa.

“Kazi  za  ukarabati  wa  majengo  na  ujenzi  wa  vyoo  ufanywa  na wajumbe wa kamati ya shule kwa kushirikina na  wanafunzi”alisema Selfu.
Mohamedi Juma mwenyekiti  wa  kamati ya  shule  hiyo  alisema wazazi  wamekuwa  wakiitafsiri  vibaya sera  ya  elimu  bure kwa kutotekeleza  maagizo  ya  vikao  vya  kamati ya  kuchangia  chakula cha  wanafunzi  na  kushiriki  kujitolea  shughuli  mbalimbali  za ukarabati  wa  majengo.

Mohamedi  alisema kukosekana  kwa huduma  ya  chakula  shuleni kuna changia kutopanda  kwa  ufaulu  hivyo  kamati  inaiomba serikali kuwachukulia  hatua  kali  wazazi  wanaogoma  kutekeleza  maagizo.
 Kwa  upande  wake  Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri ya  Kilwa Zablon  Bugingo  alisema atawaagiza  watendaji  wa  kata  na  vijiji kufanya  mikutano  ya  kuelimisha  jamii  juu  ya  dhana  ya  elimu bure.

“Serikali iliposema  elimu  bure  haikumaamisha kuwa  ni  kila  kitu ikiwemo  Sare, na chakula  mashuleni  bali  ni  gharama zile za a utoaji wa  elimu tu”  Alisema   Bugingo


 Baadhi ya  yanafunzi  wa  shule  ya msingi  Chumo wakiwa  kwenye Kikao
Diwani  kata  chumo  akizungumza  kwenye kikao  kuhusu  masuala  ya  elimu

Post a Comment

 
Top