Mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 12, badala ya mashtaka sita waliyosomewa awali.
Miongoni mwa mashtaka hayo 12 ya uhujumu uchumi yamo mashtaka matano ya kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27(USD 138,275.82).
Mashtaka hayo yanayowakabili ni pamoja na kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kuisababishia Serikali hasara na kutakatisha fedha.
Miongoni mwa mashtaka hayo ni kudaiwa, kati ya oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014 jijini Dar es Salaam ,Rugemarila na Sethi walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari 23,2014 makao makuu Benki ya Stanbic kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi la St .Joseph kwa ulaghai washtakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), walijipatia USD 22,198,544.60 na Tsh 309, 461,300,158.27.
Vilevile Sethi ,anadaiwa kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Machi 14,2014 katika tawi la kati la Benki ya Stanbic Kinondoni Dar es Salaam alitakatisha fedha,Sh 309,461,300,158.27 kutoka BOT wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Januari 23,2014 katika benki ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemarila alitakatisha fedha USD 22,000,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
Hata hivyo,washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao.
Baaada ya kusomewa mashtaka hayo, wakili Shedrack Kimaro alidai upelelezi bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi Julai14,217.
Post a Comment