0
Kufuatia Tetesi nyingi za baadhi ya wachezaji kutokuonekana tena kwa msimu huu wa 2017/2018 katika klabu ya Dar Young Africans yenye maskani yake mtaa wa Jangwani jijini Dar es salaam.
Habari zilizotufikia ni kwamba Mlinda mlango mahiri wa klabu hiyo Deo Munishi ‘Dida’yeye amemaliza muda wake wa kuitumikia klabu hiyo na sasa anajiunga na klabu ya Afrika Kusini, hayo yamethibitishwa na Katibu mkuu wa Klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa.

Japo siku za hivi karibuni Mlinda mlango huyo ameonekana katika mazoezi ya Yanga Mkwasa amesema kuwa wamemruhusu kuendelea na mazoezi ya klabu ili kulinda kiwango chake katika kipindi hiki ambacho anasubiri mambo yake yakae sawa ili ajiunge na timu yake hiyo nchini Afrika kusini.
Naye winga machachari wa Klabu hiyo Simon Msuva anatarajia kujiunga na Timu ambayo ni washindi wa pili ligi kuu nchini Morocco klabu ya Difaa Al Jadida.
Msuva amesema “Naondoka Yanga SC , timu iliyonilea na kunipa mafanikio . . Siondoki kwa ubaya ndio maana nimefuata taratibu zote ambapo viongozi wote wa pande mbili wameafikiana na kufanya biashara, naamini ipo siku ntarudi kuitumikia Yanga tena ila mpaka nitimize malengo yangu ya kucheza soka la kulipwa Ulaya na kuwa miongoni mwa wanasoka waliofanikiwa nchini, baada ya Morroco mungu akijalia basi itakuwa Ureno lakini hasa hasa ni Spain maana nna uwezo wa kucheza La Liga . . Ahsante wana Yanga kwa ushirikiano mlionipa naamini kupitia kipaji changu kuna furaha nimewapa”
katika Hatua nyingne Klabu ya Singida United imemtangaza kumsajiri aliyekuwa Golkipa wa mabingwa wa Tanzania Bara Yanga Ally Mustafa “Bartez”. Taarifa zinasema kuwa Mustafa amesaini Kandarasi ya Miaka miwili kuitumikia Klabu hiyo.

Post a Comment

 
Top