0
Msaada wa fedha kwa wakimbizi unawawezesha kujikwamua kiuchumiHaki miliki ya pichaWFP
Image captionMsaada wa fedha kwa wakimbizi unawawezesha kujikwamua kiuchumi
Serikali ya Ufaransa imechangia kiasi cha Euro 250,000 kwa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP ili wakimbizi nchini Tanzania waweze kupata msaada zaidi wa kifedha.
Msaada huu unadhihirisha mchango wa serikali ya Ufaransa katika kuhakikisha kuna hali ya usalama wa chakula.
Mwezi Desemba mwaka jana, WFP ilianza kusambaza shilingi za kitanzania 20,000 sawa na dola 9 za marekani kila mwezi kwa wakimbizi 10,000 ukiwa ni mpango wa majaribio uliotekelezwa kwa kushirikiana na washirika ikiwemo serikali ya Tanzania na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
Mchango wa Ufaransa unaiwezesha WFP kuendeleza mradhi huu wa kutoa fedha kwa wakimbizi 10,000 kwa kipindi cha miezi miwili zaidi.
Chini ya mradi huu, wakimbizi wanapokea mgao wa mafuta yatokanayo na mimea, unga kwa ajili ya uji, wakati mgao wa mahindi, na chumvi hubadilishwa kwa fedha.
Kabla ya uzinduzi wa utoaji mgao wa fedha, wakimbizi walikuwa wakipokea msaada wa chakula pekee kutoka WFP.
Wakimbizi wakichuuza bidhaaHaki miliki ya pichaWFP
Image captionWakimbizi wakichuuza bidhaa
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, asilimia 98 ya wakimbizi wanapenda zaidi kupatiwa msaada wa fedha wakati asilimia 83 wamesema zimewasaidia katika kuimarisha matumizi ya chakula na kupata aina mbali mbali za vyakula.
''Matokeo ya mpango huu wa,msaada wa fedha umekua si njia pekee inayopendelewa na wakimbizi zaidi ya msaada wa chakula lakini pia ni njia ambayo inasaidia kukuza uchumi wao,'' amesema Michael Dunford, mwakilishi wa WFP nchini Tanzania.
Miaka ya karibuni,shirika hilo limekua likiongeza kiasi cha msaada linalotoa kwa mtindo wa fedha na vocha.
Asilimia 29 ya wanaonufaika na WFP hupokea msaada wa chakula kwa njia ya fedha.
Tangu kutokee hali ya kutetereka kwa usalama nchini Burundi mwaka 2015, zaidi ya raia 250,000 wa nchi hiyo walitafuta hifadhi nchini Tanzania, ambayo sasa imewapa makazi wakimbizi 315,000, wengi wao kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ifikapo mwishoni mwa mwaka, WFP ina mpango wa kuongeza mgao wa fedha kwa wakimbizi 80,000, shirika linahitaji dola za marekani milioni 6.8 kwa mwezi kuendelea na mpango wa kutoa fedha na chakula kwa wakimbizi nchini Tanzania.

Post a Comment

 
Top