0



Mtafiti Mkuu Kiongozi Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) Leonard Mboera akizungumza kwenye mkutano wao wa Watafiti,uliohusu Utafiti kuhusu taarifa za vifo vinavyotokea katika hospitali za Tanzania,uliofanyika katika taasisi hiyo mapema leo mchana,ambapo watafiti mbalimbali walihudhuria na kuwasilicha mada zao sambamba na kuzijadili kwa pamoja.


Katika mkutano huo,Dkt Leonard alisema kuwa wamefanya utafiti wa kuangali eneo kubwa na vyanzo na sababu za vyanzo katika hospitali zetu hapa nchini,alisema kuwa katika utafiti huo vya wameufanya kwa kujumuisha hospitali ya Taifa Muhimbili,hospitali tatu za rufaa,hospitali maalum ambazo ni Kibong'oto,Mirembe,taasisi ya saratani ya ocean road,taasisi ya MOI na pia wakajumlisha hospitali zote za mikoa na asilimia kumi ya hospitali za Wilaya.

Dkt Leonard alisema kuwa dhumuni la kufanya utafiti huo ni kuangalia upatikanaji wa takwimu za vifo katika hospitali hizo na pili kuangalia ni magonnjwa gani ambayo yanasababisha vifo hospitalini "na zoezi hilo lilianza Julai 20016 na ukusanyaji wa takwimu ulikamilika mwezi Novemba,2016 ,baada ya hapo tukawa tunafanya uchanganuzi",alisema Dkt Leonard.

Alisema kuwa walichobaini katika uchanganuzi huo katika makundi ya magonjwa kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO),Magonjwa ya kuambukiza,maradhi yanawakuta Wakina mama wakati wa uja uzito na maradhi yanayohusiana na Lishe ndio yanayoongoza (kundi kubwa) kwa kuwa na asilimia 57,kundi kubwa, na Magonjwa yasiambukizwa ni asilimia 30 (kundi la kati) na kuna kundi dogo la Maradhi linalosabishwa na ajali ambalo linachukua asilimia 15.


kutokana hali hiyo Magonjwa yasio ambukiza yameanza kuchukua nafasi,lakini kwa upande mwingine ugonjwa wa Malaria ndio una oongoza kuleta vifo katika hospitali zetu.


Baadhi ya Watafiti waliokutana leo katika mkutano wao,ambao ulibeba dhima ya 'Utafiti kuhusu taarifa za vifo vinavyotokea katika hospitali za Tanzania'.

Post a Comment

 
Top