0
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
Serikali imeombwa kuangalia upya viwango vya ushuru wa mazao ya kilimo kwa vyama vya msingi vya ushirika  cha Matekwe (Matekwe AMCOS).
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake takribani 400 kati ya 525 wanaounda Matekwe AMCOS, mwenyekiti wa chama hicho, Mohamed Jafari alisema ushuru wa shilingi 50 kwa kila kilomoja ulioruhusiwa kutozwa na vyama vya msingi ni mdogo na unaviwango hicho ili vyama viweze kumudu gharama za uendeshaji wake.
Huku akibainisha kuwa kiwango hicho kinasababisha vishindwe kumudu gharama. Badala yake vinamadeni ambayo visiporekebishwa vinaweza kushindwa kulipa .Jafari alitolea mfano chama chake kudaiwa posho na wajumbe wa bodi na watendaji.“Lakini ni mara chache kuonekana korosho hazijapungua uzito kule mnadani,matokeo yake tunalazimika kufidia.Mwaka jana tulitumia shilingi milioni sita,” alisema Jafari kwa wanachama wa vyama vya msingi kuepuka majungu, tamaa na ubinafsi ambavyo vinasababisha migogoro ya mara kwa mara.
Akibainisha kuwa migogoro inachangia kushusha viwango vya mapato na uzalishaji. Nae mkuu wa idara ya ushirika ya halmashauri ya wilaya ya hiyo, Lameck Chotta aliwataka viongozi wa vyama vya ushirika kuacha ubinafsi unaosababisha wawe natamaa ya kuhujumu fedha na mali za vyama. Badala ya kutanguliza maslahi ya vyama hivyo . “Msipo angalia viongozi wa ushirika. Kwahiyo msipitie milango ya nyuma na kuingilia shuguli za ushirika,” alisema Chotta.
Chama cha msingi Matekwe ambacho kilikuwa na wanachama 525, jana kiliongeza wanachama 82, wengine waliojiunga ni waliokuwa wamehama chama hicho na kujiunga na vyama vingine.

Post a Comment

 
Top