0
 Michuano ya ligi ya Kazumari cup 2017 leo julai 31 kulikuwa na mchezo kati ya timu ya Mitumba dhidi ya Likongowele fc mchezo uliopigwa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi umemaliza kwa Mitumba fc kuibuka na ushindi wa goli 6-3 

Katika kipindi cha kwanza timu ya Mitumba fc iliongoza goli 3 kwa 1 na kipindi cha pili Mitumba fc iliongeza goli 3 na likongowele fc ikiongeza 2.

Magoli ya matatu ya Mitumba fc yalifungwa na Bakiri ng'ang'anaku,Hamza Lipupu,Shabani Mbwani na goli la sita walijifunga wenyewe Likonowele fc kupitia kwa beki wao Yahaya Ngayaga baada ya harakati ya kuokoa.

Magoli ya timu ya Likongowele fc yalifungwa na Selemani Mwigamba,Shedwaki John na goli la tatu lilifungwa na Togo Mike kwa mkwaju wa penaiti dakika ya 85.

 Mchezaji wa timu ya Mitumba fc akijaribu kumtoka beki wa Likongowele fc kwenye mchezo wa julai 31 katika uwanja wa wilaya ya Liwale.
 Mchezaji wa timu ya Mitumba fc akijaribu kumtoka beki wa Likongowele fc kwenye mchezo wa julai 31 katika uwanja wa wilaya ya Liwale.

 Mashabiki wakifuatilia mchezo kati ya Mitumba fc dhidi ya Likongowele fc
                        Goli wa timu ya Likongowele fc akipiga mpira

ANGALIA VIDEO MCHEZO KATI YA MITUMBA FC Vs LIKONGOWELE FC


Post a Comment

 
Top