0
Baadhi ya vikundi vikishika mabango wakiomba baraza la wawezeshaji kiuchumi liwaangalie wanaliwale vicoba
Kikundi kutoka kata ya  Liwale B kikiwa na ujumbe vicoba ndio mambo yote wanaliwale tujiunge na vicoba
Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Liwale, Mary Ding’hoh akitoa neno kwa wanavicoba
Wakazi wa Liwale walioudhulia kwenye maonesho ya vicoba
Mgani rasmi Mbwana Kambangwa akikagua shughuliza zinazofanywa na  kikundi cha kata ya Likongowele
   Ni moja ya kikundi kutoka kata ya Likongowele wakionyesha shughuli zao ususi na kilimo



Kikundi cha Upendo Lindota Group kutoka kata ya Nangando kikijishughulisha na ubangulishaji wa korosho,utengenezaji wa sabuni ya maji,ushonaji wa nguo,usindikaji wa unga wa muhogo pamoja na utengenezaji wa pedi asali za akina mama

Kikundi cha vicoba Chinga group kutoka kata ya Nangando kinachojishughuliza na uundaji wa mashine za kubanguaji korosho,leki na uchomeaji wa madirisha.

Kikundi cha vicoba Chinga group kutoka kata ya Nangando kinachojishughuliza na uundaji wa mashine za kubanguaji korosho,leki na uchomeaji wa madirisha, apo akijaribishia mashine ya kubangulia korosho.
Kikundi kutoka kata ya Liwale B kikiwa na bango la kumuunga mkono Rais magufuli kwa kuwatetea watanzania wanjongevinavyojishughulisha na utengenrzaji wa vyungu,kuchongaji wa mabao,vibao vya kukunia nazi.
Kikundi kutoka kata ya Liwale B vinavyojishughulisha na utengenrzaji wa vyungu,kuchongaji wa mabao,vibao vya kukunia nazi.
Vikundi kutoka kata ya Liwale mjini vinavyojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama utengenezaji wa ubuyu,keki pamoja na maandazi
Mgeni rasmi Kambangwa akipewa maelekezo kutoka kwa mwanakikundi
 Mgeni rasmi katibu tawala wilaya ya Liwale,Mbwana Kambangwa akizunguza kwenye uzinduzi wa maonyesho ya vikundi vya vicoba unaofanyika wilayani hapa kwa muda wa siku 2 julai 1 hadi julai 2

Mgeni rasmi Mbwana Kambangwa akizundua rasmi mkopa wa Vicoba
Mgeni rasmi akikoma mkoba unaosomeka Vicoba 2017 tayari kwa maonyesho rasmi ya vikundi vya Vicoba vya ujasiliamali
Ni miongoni mwa vitabu mwenye maelezo ya masuala ya vicoba vikizunduliwa julai 1 ,2017
Mratibu wa mipango vicoba endelevu,Othecla Mgumba akitoa maelezo mafupi juu ya matumizi ya vitaba mbalimbali
          Picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya wanavicoba (picha na Liwale Blog)
 
Wajasilimali wa vikundi vya Vicoba wilayani Liwale wametakiwa kushirikiana katika kufanyakazi zao ili kuweza kuleta ufanisi wa kazi hizo na pia wameshauriwa kuhifadhi bidhaa zao kwenye vifungashio maalumu  ili kuweza kuboresha bidhaa hizo.

Wito huo umetolewa jana julai 1 na mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,Mbwana Kambangwa wakati wa uzinduzi wa  maonyesho ya wajasiliamali yatakayofanyika muda  siku mbili wilayani Liwale.

Kambangwa alisema Wajasilimali wanatakiwa kujiamini  na kutambua watu wa muhimu katika ujenzi wa taifa aliongeza kusema wajasiliamani wanasaidia kuongeza teknologia katika taifa.

Awali akitoa taarifa fupi afisa maendeleo ya jamii Mary Ding’hoh alisema wilaya ya Liwale ina jumla ya vikundi vya vicoba 507 huku miongoni mwa vikundi hivyo zimewezeshwa.

Wakizungumza baadhi ya wanavikoba wa manaki,Chinga group,upendo Lindota group na upendo group wamesema moja ya changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao za ushalishaji wa bidhaa mbalimbali kama ubanguaji wa korosho,watengenezaji wa ubuyu na keki ni kukosefu wa vifungashio maalumu pamoja na kukosa soko la uhakika la kuuzia bidhaa hizo.

Pia wanavikoba hao wametoa wito wa wanawake wilayani hapa kuweza kujiunga na vicoba ili kuweza kujifunza  masuala ya ujasiliamali na kuweza kujipatia kipato.


Mratibu wa mipango vicoba endelevu,Othecla Mgumba alisema licha ya vikundi hivyo kukabiliana na changamoto za vifungashio ipo haja ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuhifadhi bidhaa katika vifungashio maalumu ili kuleta ubora zaidi wa bidhaa na kusaidia kujitangaza zaidi.

Post a Comment

 
Top