0
Mchezaji wa timu ya Market fc akimiriki mpira na kutoa pasi 

 Mchezaji wa timu ya Sido fc,Abu Kazumari akimiriki mpira kwenye mchezo dhidi ya Market fc wa ufunguzi wa ligi ya Kazumari cup 2017



Chama cha mpira wa miguu wilaya ya Liwale mkaoni Lindi (LIDIFA),leo imetangaza julai 2017 kuwa tarehe rasmi ya kuanza kwa Ligi ya Kazumari Cup 2017 na kuthibitisha timu 11 zitakazo shiriki ligi hiyo.

Timu zinazoshiriki ni Sido fc,Market fc,Mifugo fc,Mitumba fc,Vijuso fc,Mbaya city,Nyera city,Storaway fc,New generation,Likongowele fc na Wachukuzi fc.

Katika mchezo wa kufunguzi wa pazia la ligi ya Kazumari Cup kulikuwa na mchezo kati ya timu ya Sido fc dhidi ya Market fc umemalizika kwa timu ya Sido fc kuibuka na ushindi wa goli 5-0,mchezo ulipigwa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza Sido fc iliongoza magoli bila na kipindi cha pili iliongeza goli 3 ikiwa goli mmoja Market fc walijifunga wenyewe mpira alioshindwa kuokoa Ngwadiliro Ngossa na magoli manne yakifungwa na Abu Kazumari,Omari Kijuwineke,Mustapha Himbu na Salmin Mmuka.

Julai 23 kutapigwa mchezo mmoja unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kati ya timu ya Mifugo fc dhidi ya Mitumba fc majira ya saa 10 jioni katika uwanja wa wilaya ya Liwale.


Katibu wa cha chama cha Lidifa Nourdin Kazumari alisema ligi ya Kazumari cup imefadhiliwa na mfanyabiashara wa vifaa vya umeme maarufu kama Kazumari Shop. 

ANGALIA VIDEO YA GOLI YA SIDO FC 

Post a Comment

 
Top