0
Maseneta wengine wawili, Rand Paul na Susan Collins tayari walikuwa wametangaza kuupinga musawada huo.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaseneta wengine wawili, Rand Paul na Susan Collins tayari walikuwa wametangaza kuupinga musawada huo.
Maseneta wengine wawili wa chama cha Republican wanasema kuwa wanapinga mpango wa chama chao, wa kuubadilisha muswada wa afya wa Obamacare hatua iliowawacha viongozi wa Republican na uchache wa kura kufanya mabadiliko hayo.
Mike Lee na Jerry Moran wote walitangaza kwamba hawawezi kuunga mkono muswada huo kama ulivyo.
Viongozi wa Republican wanashikilia viti 52 katika bunge hilo lenye wanachama 100, na huku wanachama wawili wa Republican wakiupinga muswada huo hawangeweza kuruhusu viongozi wengine kuupinga.
Rais Trump aliahidi kuubadilisha muswada wa afya wa rais Obama kama ahadi yake wakati wa kampeni
Maseneta hao wawili walitangaza hatua yao mara moja.
Huku wakisema kuwa kulikuwa na matatizo mbalimbali kuhusu muswada wa Obamacare, waliongezea kuwa ''hawawezi kuidhinisha sera mbaya''.
Hatua hiyo inaendeleza kuwatoza kodi muhimu matajiri huku ikiwaondolea mzigo watoaji huduma za bima ili kuweza kuwapunguzia malipo watu masikini wanaohitaji huduma ya afya.
Mike Lee na Jerry Moran wote walitangaza kwamba hawawezi kuunga mkono muswada huo kama ulivyo.Haki miliki ya pichaNASA
Image captionMike Lee na Jerry Moran wote walitangaza kwamba hawawezi kuunga mkono muswada huo kama ulivyo.
Maseneta wengine wawili, Rand Paul na Susan Collins tayari walikuwa wametangaza kuupinga musawada huo.
Democrats walikuwa wamesema kuwa hawatakubali kuubadilisha muswada huo wa Obamacare lakini wanaweza kufanya kazi kwa pamoja ili kuufanya kuwa imara.
Viongozi wa Republican na ikulu ya Whitehouse sasa watalazimika kuamua iwapo watauandika upya mpango huo ama kuanzisha juhudi mpya bila kupendelea chama chochote kuangazia matatizo yaliopatikana na vyama vyote viwili katika muswada wa Obamacare, ama kuangazia maswala mengine kama vile mabadiliko ya kodi.
Akiongea kuhusu kile kimetajwa kuwa pigo kubwa ,rais Trump amewataka Republicans kuubadilisha muswada huo wa Obamacare na kuanza juhudi za kutengeza muswada mwengine wa afya ambao utaungwa mkono na Democrats.
Bunge la seneti limekuwa likichelewesha likizo yao kwa lengo la kubadilisha muswada huo wa aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama.

Post a Comment

 
Top