0

Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
HALMASHURI ya wilaya ya Nachingwea kupitia idara yake ya ushirika imetajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha mgogoro kwenye vyama vya msingi vya ushirika.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya Wanachama wa chama cha msingi cha Matekwe, kwenye mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika leo katika kijiji cha Kilimarondo. akichangia kwenye mkutano huo, mwanachama na mkulima Thabiti Magoja alisema idara ya ushirika ya halmashauri hiyo ni miongoni mwa sababu zinachangia migogoro kwenye baadhi ya vyama vya msingi wilayani humo.
Magoja aliyekuwa anazungumza na kuungwa mkono na wanachama wenzake walikuwepo ndani ya ukumbi. Alisema mwenendo wa Halmashauri hiyo kupitia idara yake ya ushirika unaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
“Tunajua kwamba kuanzisha chama havipungui vikao sita ndipo chama kipya kinaanzishwa lakini waliojitoa wameanzisha chama baada ya vikao viwili tu, nyie mlipata nini,” alihoji Magoja.
Mkulima huyo alisema halmashauri hiyo iliazimia kuwa hakutakuwa na usajili wala kuanzishwa chama kipya cha msingi ndani ya halmashauri hiyo. Hata hivyo vyama vinaendelea kuanzishwa na kutambuliwa na halmashauri hiyo.
“Kama kuna mnachopata mjue mnatuumiza wengi, tutachoka tutawalipueni. Mgogoro ule umesababisha tushindwe kutumia ghala letu hadi mazao yananunuliwa kwenye maeneo hatarishi, nguvu za kuzuia tusitumie ghala letu wale wenzetu wanapata wapi kama sio kwenu. Sababu hatuoni hatua zinazochukuliwa na ofisi ya idara ya ushirika ,” alisema Magoja.
Akijibu malalamiko hayo makamo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Isaya Ndwewe licha ya kushangaa wakulima na lawama hizo, alisema halmashauri haina uwezo wa kuzuia vyama vya ushirika kusajiliwa kwasababu ni jambo lilipo kisheria. Nakubainisha kuwa hata azimio la halmashauri linadumu na kuwa halali kwa muda wa miezi sita tu. Hivyo halmashauri kupitia idara yake ya ushirika haina uwezo wa kuzuia wala kusajili vyama vya msingi.
“Hakuna chama kilichosajiliwa wala kuanzishwa kufuata taratibu, kanuni wala sheria zilizopo. Pia nivema kabla ya kulaumu mjue taratibu, kanuni na sheria za hicho uliofanyika unachojaribu kujaribu kulaumu kwa ujasiri ,” alisema Ndwewe.
Aidha aliwaasa wanasiasa waache kuingilia mambo yanayohusu ushirika na kupotosha mambo kwa masilahi ya kisiasa kwa kupingana na maagizo sahihi ya mamlaka na wataalamu. Mkutano huo pia ulitumika chagua viongozi wa chama hicho, ambapo Mwenyekiti aliyekuwa amemaliza muda wake, Mohamed Jafari alichaguliwa tena kwa nafasi hiyo.

Post a Comment

 
Top