0
Chelsea imemsajili Tiemoue Bakayoko kwa kandarsi ya miaka 5
Image captionChelsea imemsajili Tiemoue Bakayoko kwa kandarsi ya miaka 5
Chelsea imemsajili kiungo wa kati Tiemoue Bakayoko kutoka klabu ya Ufaransa ya Monaco kwa kitita cha fedha kisichojulikana.
Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 ametia saini kandarasi ya miaka mitano na mabingwa hao wa ligi ya Uingereza.
Ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Chelsea baada ya hapo awali kumsajili beki Antonio Rudiger kutoka Roma.
Bakayoko alijiunga na Monaco kutoka klabu ya ligi ya dara la kwanza Rennes 2014 na kuchezeshwa mara kwanza katika timu ya taifa katika mechi dhidi ya Uhispania mwezi Machi ambapo Ufaransa ilipoteza mwaka huu.
Alikuwa miongoni mwa kikosi cha Monaco kilichofika nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu uliopita baada ya kubanduliwa na Juventus.
Bakayoko ambaye atavalia jezi nambari 14 akiwa Chelsea alisema:Nafurahi sana kuwa hapa na kujiunga na timu hii.
''Nimekuwa nikiangalia Chelsea.Kusaini mkataba lilikuwa swala la kawaida kwa sababu ni klabu nilioipenda utotoni mwangu''.

Post a Comment

 
Top