0

Mwenyekiti  wa  chama  cha  walimu (CWT)  mkoa  wa  Lindi,Mlami  Seba,wakati anafunga mafunzo ya kuwajengea  uwezo  viongozi  wa  Asasi  za  kijamii  na wawakilishi  wa  Chama hicho,yaliyofanyika mji mdogo wa Masoko,wilaya ya Kilwa.


 MWAANDISHI  WETU  KILWA
:SERIKALI imeombwa kuongeza jitihada katika kutatua changamoto zinazoikabiri sekta nya elimu,ikiwemo kuboresha miundombinu ya majengo,vitabu na madai ya walimu,ili kuwezesha utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi.
 
Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti  wa  chama  cha  walimu (CWT)  mkoa  wa  Lindi,Mlami  Seba,wakati anafunga mafunzo ya kuwajengea  uwezo  viongozi  wa  Asasi  za  kijamii  na wawakilishi  wa  Chama hicho,yaliyofanyika mji mdogo wa Masoko,wilaya ya Kilwa.
 
Mafunzo hayo ya siku tatu yaliandaliwa  na    Mtandao  wa  Elimu Tanzania (TENMET) kwa  ushirikiano na  Action Aid na Asasi  za Kiraia ya wilaya  Kilwa  (KINGONET) yalihussisha pia na elimu ya mlipa kodi.
 
Seba akifunga mafunzo hayo amesema kitendo cha kutoboreshwa kwa miundombinu,ikiwemo nyumba za kuishi watendaji wake (walimu), kukosekana kwa vitendea kazi vya kutosha (vitabu) ni sehemu ya changamoto zinazosababisha hali ya elimu katika sekta hiyo kuendelea kudumaa,hali inayowakatisha tama.
 
Amesema serikali kupitia sera ya elimu bure,imesaidia kupunguza kero ya wanafunzi kuketi sakafuni kwa kusambaza madawati mashuleni,jambo lililosaidia ongezeko la wazazi na walezi kupeleka Shule watoto wao wapate elimu ile iliyo bora.
 
Mwenyekiti huyo wa (CWT) mkoa wa Lindi,pia ameiomba Serikali kushirikiana na Jamii kuhakikisha changamoto zinazowakabiri walimu,kama vile upatikanaji wa vitendea kazi (vitabu),vyumba vya madarasa,vyoo na nyumba za kuishi zinapatikana,ili kuwapunguzia kero watendaji wa Idara hiyo.
 Amesema uwamuzi uliofanywa na mtandao wa Elimu Tanzania (TANMET) kwa kushirikiana na Action Aid na Kingonet wilaya ya Kilwa,kutoa elimu kwa walimu na Asasi za kijamii mambo mbalimbali,ikiwemo kuelimisha sera hiyo bure.
 
Mwanzoni Afisa Mradi wa TANMET,Anastilia  Kamgisha ambaye pia alikuwa ni miongoni mwa wawezeshaji,alisema mafunzo  hayo yamelenga  kuwapatia  elimu wadau  kuhusu   haki zinazowahusu watoto  mashuleni,pamoja  na  umuhimu  wa  kukusanya   mapato  ya serikali,kwa  ajili  ya  utoaji  huduma   mzuri kwa jamii na  elimu iliyo bora  kwa watoto

Post a Comment

 
Top