Mwandishi mmoja wa habari amepigwa na risasi kimakosa shingoni wakati akifuatilia mapigano nchini Ufilipino.
Adam
Harvey anayefanya kazi na kituo cha ABC alichapisha picha ya X-ray
katika mtandao wa Twitter ya risasi iliyokwama ndani ya shingo lake.Hata hivyo jera hilo sio la kumtishia maisha, mkurugenzi wa ABC alisema.
- Jeshi la Ufilipino laahidi kushinda vita dhidi ya waasi
- Mji wa Marawi nchini Ufilipino wavamiwa na IS
Kuna ripori kuwa baadhi ya wakazi bado wamekwama mjini humo.
Mwanasiasa mmoja amesema kuwa wale ambao wamefanikiwa kuondoka wameripoti kuona maiti nyingi za watu waliouawa kwenye mapigano kati ya wanamgambo na vikosi vya usalama.
Bwana Harvey anasema alikuwa akiinama kuchukua chakula kutoka kwa gari akiwa amevalia mavazi ya kujinga dhidi ya risasi, wakati aligonjwa na kitu alichohisi kuwa ni kama mpira wa kriketi.
Alipewa huduma ya kwanza akifikiri kuwa labda alikuwa amegongwa na ganda la risasi, lakini wakati aliamua kutibiwa picha za X-ray zilionyesha alikuwa amepigwa risasi.
Post a Comment