Mamlaka
ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kwa kushirikiana Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel kupitia application ya VSOMO leo wametangaza na
kuzindua kozi mpya za ufundi stadi za VETA zitakazotolewa kupitia simu
za mkononi ili kuwawezesha watanzania kujiunga na kupata utaalamu na
vyeti vya VETA kwa gharama nafuu
Kozi
hizo mpya zinazoongezwa katika mfumo wa vsomo ni Huduma ya chakula na
mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani,
ufundi Bomba wa Majumbani na Umeme wa magari.
Tangu
kuzinduliawa kwa mfumo huu wa mafunzo kwa njia ya mtandao kupitia
application ya VSOMO mwezi wa Juni 2016 ulianza kutoa kozi mbalimbali za
ufundi za VETA ikiwemo Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki,
Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya
urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano, akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kozi tano mpya kwenye awamu ya
pili ya mpango wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu ya
VSOMO inayoratibiwa na kampuni ya Airtel. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa VETA, Dk. Bwire Ndazi.
Lengo
la mfumo huu likiwa ni kutimiza dhamira ya VETA ya kutanua wigo wa
mafunzo ya ufundi stadi nchini na kuongeza idadi ya vijana kujipatia
fani mbalimbali za ufundi ili waweze kuajirika au kujiajiri. Mafunzo
haya yanawawezesha wanafunzi kujisomea wakati wowote kwa gharama nafuu
kupitia simu zao za mkononi za Airtel.
Mfumo
huu wa masomo kwa njia ya Mtandao VSOMO, sasani maarufu kwa vijana
ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua
application ya VSOMO, 8000 wamejiandikisha na kati yao 50 wanasoma kozi
mbalimbali zilizopo pia wapo waliomaliza na kupata vyeti vya VETA.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa kozi tano mpya kwenye awamu ya pili ya
mpango wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu ya VSOMO
inayoratibiwa na kampuni ya Airtel, Dar es Salaam jana.Kushoto ni
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano.
Akiongea
wakati wa kuzindua na kutangaza kozi hizo, Mkuu wa chuo cha Veta
Kipawa, Eng. Lucius Luteganya alisema “mafunzo ya ufundi kwa njia ya
mtandao ya VSOMO yametuwezesha kuongeza wigo na kuwafikia watanzania
wengi nchini. Tunaamini bado tunayofursa ya kuongeza wigo zaidi na
kuongeza idadi ya vijana wenye ueledi ili kwenda sambamba na agenda ya
serikali ya awamu tao ya uchumi wa viwanda kwa kupata nguvu kazi yenye
taaluma muhimu katika kuendesha uchumu wa nchi”
“Tunaamini kozi hizi mpya zitatawavutia vijana wengi kujiandikisha, kusoma na kupata ujuzi zaidi.” Alisisitiza Eng Luteganya
Eng,
Luteganya alisema kuwa “Ili kupata mafunzo ya VSOMO kupitia Airtel,
ukiwa na Airtel pakua application katika google play store, na
kujisajiri na kisha chagua kozi inayokidhi mahitaji yao.
ili
kuhakikisha tunasimamia viwango vya elimu vilivyowekwa na VETA, wale
watakaomaliza masomo yao nadharia kupitia VSOMO watafanya mtihani ili
kufaulu na kujiunga na mafunzo ya vitendo katika vituo vya VETA
vilivyopo nchi nzima. Vyeti vya kuhitimu mafunzo vitatolewa kwa wale
watakaofaulu mafunzo katika hatua zote mbili ya nadharia na vitendo”.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akionyesha jinsi ya kutumia
simu ya mkononi kupata progaramu ya masomo ya mafunzo ya ufundi Stadi
VSOMO wakati wa uzinduzi wa programu ya pili ya mfunzo hayo jana.Kushoto
ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano na
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam,Habib Burko.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano
Mallya alisema “Tunajisikia furaha kuongeza kozi nyingi zaidi katika
mfumo huu wa masomo kwa njia ya mtandao wa VSOMO kwani itatuwezesha
kufikia idadi kubwa ya vijana wanaosoma kwa kupitia simu zao za mkononi.
Lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na kozi nyingi ili kwenda sambamba
na matarajio na mahitaji ya wanafunzi na watanzania kwa ujumla”.
Tunapenda
kuwapongeza wote waliojiunga na kumaliza kozi zao na kuhimiza wote
ambao hawajapakua application ya VSOMO kufanya hivyo kwa kujiandikisha
katika mojawapo ya kozi 12 zinazopatikana katika application ya VSOMO
kwa gharama nafuu ya shilingi 120,000 tu na kulipia kwa njia ya Airtel
Money kwa kupiga *150*60#.
Tunapenda
kuwahimiza vijana kutumia fursa hii na kujiunga na kozi na kujisomea
wakati wowote na mahali popote. kozi hizi zinazochukua hadi mienzi
mitatu kumalizika lakini pia zinaweza kuisha mapema kulingana na muda
utakaotengwa na mwanafunzi kuweka bidii ili kumaliza mapema.
Post a Comment