Utawala wa rais
Trump umeweka masharti mapya ya maombi ya Visa kutoka kwa mataifa sita
ya Kiislamu pamoja na wakimbizi wote, ambayo yanawataka kuwa na mtu
wanaohusiana ama ushirikiano wa kibiashara na Marekani.
Hatua hiyo
inayoyahusisha mataifa yalio na Waislamu kama vile Iran,
Libya,Somalia,Sudan ,syria na Yemen imeangaziwa katika ujumbe uliotumwa
katika balozi zote.Masharti hayo mapya yalioanza kufanya kazi siku ya Alhamisi yanaelezea mahusiano ya kifamialia kama mzazi, mkeo ama mumeo,mtoto wa kiume ama wa kike.
Masharti hayo yanajiri baada ya mahakama kuu nchini Marekani kuidhinisha kwa muda agizo la rais Trump ambalo lilikosolewa kuwa marufuku kwa Waislamu.
Post a Comment