0

 
Mitungi ye gesiikisafirishwa
Mitungi ye gesiikisafirishwa
Serikali ya Tanzania imelalamika kuhusu hatua ya Kenya kukataa kuruhusu wafanyibiashara wa Tanzania kuuza gesi ya kupikia nchini Kenya.
Kulingana na taarifa iliotolewa na katibu wa kudumu katika wizara ya biashara na uwekezaji Profesa Adolf Mkenda, serikali imegundua kupitia vyombo vya habari mjini Nairobi kwamba Kenya imepiga marufuku uingizaji wa gesi ya kupika kutoka Tanzania kupitia mpaka wa Kenya na Tanzania.
Profesa Mkenda alisema hatua hiyo ya Kenya ni kinyume na makubaliano ya jamii ya Afrika mashariki na makubaliano yalioafikiwa na mataifa hayo mawili baada ya taifa hilo kuiwekea marufuku Tanzania mnamo mwezi Mei 18, 2017.
Kulingana na Profesa Mkenda, hatua hiyo ya Kenya itaathiri wafanyibiashara wakubwa wa kibinafsi na raia wa kawaida ambao hujipatia kipato kupitia biashara ya kuuza gesi .
Alisema kwamba wakati wa mkutano wa Jamii ya Afrika mashariki ambao uliwaleta pamoja mawaziri wa biashara na viwanda swala hilo lilijitokeza.
Amesema kuwa iliamuliwa wakati wa mkutano huo ambao ulifanyika mwezi Juni tareh2 2017 kwamba Kenya ilifaa kuondoa marufuku ili kuafikia makubaliano hayo ya Afrika mashariki.
Wakati wa mkutano huo Kenya ilikubali kuondoa marufuku ya ununuzi wa gesi kutoka Tanzania kupitia mpaka wa mataifa hayo mawili.
Mbali na marufuku hiyo Kenya pia imeiwekea Tanzania marufuku ya ununuzi wa ngano swala ambalo kulingana na Mkenda ni kinyume na makubaliano ya biashara ya Afrika Mashariki.
Hatahivyo amesema kuwa serikali itaendelea na mpango wa kutatua tatizo hilo.
Hatahivyo katibu huyo hakusema ni hatua gani zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania kufikia sasa.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Siku ya Jumatatu katibu maalum nchini Kenya Andrew Kamau alisema kuwa wafanyibiashara hawataruhusiwa kununua gesi kupitia mipakani katika kipindi cha juma moja.
Hatua hiyo kulingana na Kamau ililenga kuzuia kampuni haramu zinazouza gesi ambazo zimeathiri usalama wa taifa hilo.
Katibu huyo aliandikia barua shirika linalodhibiti kawi na shirika la ukadiriaji ubora wa bidhaa KBS na kusema kuwa gesi yoyote ya kupikia inayoingia nchini ni sharti ipitie Mombasa ili kubaini ni wafanyibiashara gani ambao hawana kibali cha kuendesha biashara hiyo.

Post a Comment

 
Top