0

 
Unga wa Mahindi
Unga wa Mahindi
Tanzania imepiga marufuku uuzaji wa nje wa chakula chake kwa mataifa jirani.
Wikendi iliopita mamlaka ilikamata malori 10 ya chakula yaliodaiwa kuelekea nchini Kenya katika eneo la Terekea Kaskazini mwa Tanzania.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameonya kuwa ulanguzi wa chakula nje ya taifa hilo unatishia usalama wa chakula nchini humo.

''Kuanzia leo, yeyote atakayepatikana anasafrisha chakula kutoka nchini kuelekea nchi jirani , chakula hicho kitachukuliwa na kupelekwa katika hifadhi ya kitaifa na lori lililotumika kusafrisha mzigo huo litakabidhiwa maafisa wa polisi'', alisema.

''Serikali haitaruhusu uuzaji huo hususan wa unga wa mahindi kwa sababu utasaidia viwanda vya kitaifa''.
Aliongezea kuwa wafanyibiashara wanapaswa kuchukua vyakula kule ambako vimesheheni na kuviuza kule ambako kuna upungufu.

Kenya imekumbwa na uhaba wa chakula hususan unga wa mahindi ,ambacho ndio chakula kinachotegemewa sana afrika mashariki.

Hali hiyo imefungua fursa ya soko jipya miongoni mwa wafanyibiashara wa Tanzania.

Post a Comment

 
Top