0

Mtu mmoja amechomwa moto na kufariki dunia wilaya ya Liwale mkoani  Lindi usiku wa jana kuamkia leo ijumaa juni 30 katika kata ya Liwale mjini.

Kamanda wa polisi wilayani Liwale,Edward Malogo akizungumza na Liwale Blog amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amemtaja mtu huyo aliyochomwa moto ni Yasini Abdala  (maarufu kama Nyoka).

Kamanda wa polisi amesema  kwa madai ya tuhuma ya  kuhusika na vitendo wa wizi kwa muda mrefu huku akiongeza kusema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana  na  uchunguzi unaendelea juu ya tukio hilo.

Kamanda wa polisi amelaani kutokea kwa tukio hilo na ametoa wito kwa raia kuacha kujichukulia sheria mkononi ambao wanakuwa na taarifa ya mtu anayejihusisha na wizi ni vema wakaripoti kwenye kituo cha polisi na hata pale wanapomkamata kwa tukio fulani wanatakiwa kushirikiana na kituo cha polisi na kushirikiana kutolea ushaidi mahakamani.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi,Renata Mzinga akizungumza na Liwale Blog amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wilayani Liwale na ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa ya wahalifu kwa jeshi la polisi ili kuweza kuwachukulia hatua za sheria.

SIKILIZA AUDIO YA KAMANDA WA POLISI WILAYA YA LIWALE NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA LINDI.

Post a Comment

 
Top