Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga amewataka wanawake wa Wilaya hiyo
kuachana na masuala ya utegemezi kwa wanaume na zaidi wajikite katika
kujiendeleza kiuchumi kwa kuanzisha miradi midogo midogo ikiwemo
kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ikiwa ni katika kutekeleza maagizo
ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya
kujiinua kiuchumi..
Amesema
hayo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika
jana na kuvikutanisha zaidi ya vikundi 30 kutoka Wilaya ya Mkuranga na
kuelezea matatizo wanayokumbana katika vikundi vyao.
Sanga
amewaambia kuwa wanawake bila kuwezeshwa wanaweza wakajiendeleza
wenyewe kwani utakapomuelimisha mwanamk mmoja utakuwa umeelimisha watu
wnegi sana.
"wanawake
mkijiwezesha wenyewe mnaweza sio lazima muwezeshwe kwani tunachoamini
ni kuwa ukimuelimisha mwanamke umeelimisha dunia kwani nyinyi ndiyo
msingi mkubwa wa familia katika jamii zinazotuzunguka mtakapoamua kukaa
na kutokujishughulisha basi hakutakuwa na msingi mzuri wa kizazi
kijacho,"amesem Sanga.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji WanawakeWilaya ya
Mkuranga Mariam Ulega alisema kuwa anashukuru sana kwa Mkuu wa Wilaya
kuja kuwazindulia jukwaa lao na cha zaidi kwa kuwa wameshapatikana
viongozi wa Jukwaa hilo kwa wilaya ya Mkuranga na zaidi anaomba umoja na
ushirikiano kutoka kwa wakina mama kutoka kata mbalimbali ili kufanya
kazi kwa ushirikiano mkubwa.
Kabla ya kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ulifanyika uchaguzi na kupatikana kwa Mwenyekiti Mariam Ulega.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akizindua Jukwaa la Uwezeshaji
wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana na masuala ya
utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua kiuchumi na pia
kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika kutekeleza
maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na
vikundi vya kujiinua kiuchumi.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega
akizungumza na wakina mama wa wilaya hiyo kutoka kata mbalimbali
kuhusiana na kuviendeleza vikundi vyao kwa ajili ya kuacha kuwa tegemezi
kwa wanaume ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama
Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akipokea maandamano ya wakina mama wa Mkuranga wakati wa uzinduzi wa Jukwaa
la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana
na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua
kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika
kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya
kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akisaini kitabu cha wageni wakati alivyowasili katika uzinduzi wa Jukwaa
la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana
na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua
kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika
kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya
kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akioneshwa baadhi ya bidhaa
zinazotengenezwa na wakina mama hao wa Wilaya ya Mkuranga kutoka katika
Vikundi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Jukwaa

Post a Comment