Mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe.Sarah Chiwamba baada ya kukata utepe na kumkabidhi funguo ndugu Musa Mkoyage
ndugu Musa Mkoyage akiwa amebanda na kuliwasha trekta
Ndugu Musa Mkoyage akipongezwa na baadhi ya wafanyabiashara na wakulima walioudhulia hafla fupi hilyo
Ndugu Musa Mkoyage akipongezwa na baadhi ya wafanyabiashara na wakulima walioudhulia hafla fupi hilyo
Ndugu Musa Mkoyage akingoja kukabidhiwa trekta yake
Wa kwanza kutoka kushoto ni Meneja wa banki ya nmb huduma kwa mteja,Mwalimu Yesaya Mbwambo ,wa katikati ni Ndudu Musa Mkoyage na wa mwisho Mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe. Sarah Chiwamba. (Picha na Liwale Blog)
Banki ya NMB tawi la wilayani Liwale, mkoani Lindi imeendelea kuwahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji zaidi kupitia nchi ya viwanda kwa kumkopesha trekta 1,mkulima ndugu,Musa Mkoyage lenye thamani ya shilingi 68,500,000.
Akikabidhi trekta hilo leo juni 22, Mkuu wa wilaya wa Liwale,mhe. Sarah Chiwamba, alisema kuwa hatua ya kukabidhi trekta hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutimiza dhana ya nchi ya viwanda .
Hivyo alisema kuwa wilaya ya Liwale ni moja kati ya wilaya ambayo imekuwa ikitegemea kwa uzalishaji wa mazao ya biashara ikiwemo korosho pamoja na chakula na hivyo lazima wakulima kuendelea kuhamasishwa zaidi ili kujitokeza kukopa kwa Taasisi ya MNB ili kuweza kunufaika na mkopo ili kuweza kumuunga mkono Rais juu ya kuweza kutimiza sera ya nchi ya viwanda.
Pia Mkuu wa wilaya alitumia nafasi hiyo aliwataka wakulima walioudhulia hafla hiyo ya kumkabidhi trekta ndugu Mkoyage ambaye amekopeshwa trekta hilo mbali ya kutumia katika kilimo cha zao la korosho pia kuhakikisha analima hata mazao ya chakula kwa wingi ili kuendelea kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula katika wilaya ya Liwale.
Meneja wa banki ya nmb huduma kwa mteja,Mwalimu Yesaya Mbwambo alisema kuwa mkulima huyo amejitokeza kuchukua mkopo huo wa trekta jipya HP 60 ambapo banki imemkopesha asilimia 75 ya shilingi 68,500,000 kwa kuwa alikuwa akinyanyasika zaidi kwa kilimo cha jembe la mikono hivyo kupitia trekta hilo sasa litaweza kumwongezea uzalishaji zaidi.
Meneja Mbwambo alisema mkopo huo wa trekta una riba ya asilimia 19 na muda wa kulipa mwaka hadi miaka 3 pia aliweza kulielezea sifa na vitu ambavyo zimeambatanishwa kwenye trekta hilo kuwa trekta ni jipya,lina nguvu kubwa ya HP 60,tela lake linauwezo wa kubeba tani 12 na inauwezo wa kubinua,lina four wheel Drive,majembe pamoja lina bima kubwa.
|
Kwa upande wake ndugu Musa Mkoyage mara baada ya kukabidhiwa trekta hilo alisema mkopo huo wa trekta utaweza kuleta tija katika kuweza kuondokana na kilimo cha jembe la mkono hivyo sasa ataweza kulima kwa wakati na kuweza kuongeza uzalishaji.
Mkoyage alitumia hafla hiyo kuwaomba wakulima walioudhulia kuweza kumunga mkono kushirikiana nae katika kuweza kuwahudumia kwenye mashamba yao pia aliwaondoa wasiwasi wakulima wezake kuondokana na dhana kuwa mikopo inakupelekea kwenye matatizo aliwambia kuwa mkopo ni malengo na endapo mkopo utaubadilishia malengo au matumizi itapelekea kuyumba na kushindwa kurejesha mkopo na kutapata matatizo.
Akizungumza kwa niaba ya walima na wafanyabiashara walioudhulia kwenye hafla hiyo, Bwana Theophil Nnenjela aliipongeza banki ya NMB kwa kuweza kukopesha trekta hilo na sasa banki hiyo imefungua milango kwa wakulima kuweza kupata mikopo mbalimbali ili kuweza kujiinua kiuchimi na akiomba banki hiyo kutoa mikopo yenye masharti nafuu pamoja na riba ndogo.
Ndugu Musa Mkoyage aliyekaa upande wa kushoto akiwa na Meneja wa banki ya nmb huduma kwa mteja,Mwalimu Yesaya Mbwambo
Baadhi ya wakulima na wafanyabiashara walioudhulia kwenye hafla fupi ya kumkabizi ndugu Musa Mkoyage trekta iliyofanyika eneo la banki ya NMB wilayani Liwale.
Baadhi ya wakulima na wafanyabiashara walioudhulia kwenye hafla fupi ya kumkabizi ndugu Musa Mkoyage trekta iliyofanyika eneo la banki ya NMB wilayani Liwale.
Akizungumza kwa niaba ya walima na wafanyabiashara walioudhulia kwenye hafla hiyo, Bwana Theophil Nnenjela.
ANGALIA VIEO JINSI MKULIMA ALIVYOFURAHIA KUPATA TREKTA HIYO
Post a Comment