Mke wa waziri mkuu aliyechaguliwa nchini Lesotho ameuwawa siku mbili kabla ya kuapishwa kwake.
Polisi
wanasema mke wa Thomas Thabane, Lipolelo, ambaye walikuwa wametengana
aliuwawa hapo jana Jumatano wakati akiendesha gari karibu na nyumbani
kwake, katika mji mkuu wa Maseru.
Hawajakuwa wakiishi pamoja tangu mwaka 2012, baada ya Bwana Thabane kuwasilisha kesi ya talaka mahakamani.
Lesotho imekuwa na historia ya migogoro ya kisiasa.
Mnamo mwaka mwaka 2014 wanajeshi walijaribu kumpindua Bwana Thabane, pale alipokuwa waziri mkuu.
Lipolelo
alishinda kesi dhidi ya mumewe wakati akiwa waziri mkuu, akitaka akuwe
na cheo cha mama wa taifa, baadala ya mke wake mdogo Liabiloe Thabane.
Uchaguzi
ulifanyika nchini Lesotho mapema mwezi huu na ndio wa tatu katika
kipindi cha miaka mitatu kutokana na mgogoi mbaya wa kisiasa.
Bwana Thabane ataapishwa siku ya Ijumaa
Post a Comment