Gwiji wa ndondi
duniani Floyd Mayweather atazipiga na bingwa wa UFC Conor McGregor
katika pigano lililoelezewa kuwa la ''vinyago na sarakasi'' lakini
linaweza kuwapatia wawili hao kima cha dola milioni 100 .
Mmarekani
Mayweather mwenye umri wa miaka 40 alichapisha kanda ya video katika
mtandao wa twitter akithibitisha kuhusu pigano hilo litakalofanyika
mjini Las vegas mnamo tarehe 26 Agosti yenye ujumbe ''sasa ni rasmi''.
Atamkabili Mayweather akipanga kumpiga 'Knockout'.
UFC ni pigano ambalo linashirikisha ndondi na miereka.
- Mayweather avunja pigano na nyota wa UFC
- Bondia anayefuata nyayo za Mayweather ahifadhi taji lake
- Manny Pacquiao arudi ulingoni na ushindi
Bingwa huyo wa Ireland mwenye umri wa miaka 28 naye alithibitisha akisema pigano hilo litafanyika.
Rais wa UFC Dana White aliambia chombo cha habari cha ESPN: makubaliano yaliokuwa magumu yameafikiwa.
Pigano hilo la uzani wa Middleweight litakuwa lenye thamani kubwa duniani katika historia ya masumbwi.
Mayweather,
ambaye ni bingwa wa zamani katika mizani mitano tofauti na ambaye
anajulikana kuwa bondia bora wa kizazi chake alistaafu mwaka 2015 baada
ya mapigano 49 bila kushindwa.
Aliwahi kutetea taji lake la WBC
na WBA, mafanikio ambayo yalimwezesha kuifikia rekodi iliowekwa na Rocky
Marciano ya mapigano 49-0.
Mayweather alistaafu kwa mara ya kwanza 2008 baada ya mapigano 39.
McGregor
ambaye hajawahi kupigana ndondi za kulipwa alifanikiwa kuwa bingwa wa
UFC mnamo mwezi Novemba 2016 na amekuwa akimtaka Mayweather kupigana
chini ya sheria za pigano linaloshirikisha ndondina miereka.
Post a Comment