0


Mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe. Sarah Chiwamba (kushoto) akimkabidhi bibi zawadi ya chakula kwa ajili ya sikukuu ya idd el fitri.
Mkuu wa wilaya ya Liwale akiwa na baadhi ya akina mama waliweza kupata msaada siku ya jumamosi 24 mwaka 2017.
Mkuu wa wilaya ya Liwale akiwa na baadhi ya akina mama waliweza kupata msaada siku ya jumamosi 24 mwaka 2017.
     Kaya zilizofika kupokea msaada wa chakula kwa ajili ya sikukuu ya idd el fitri
Mkuu wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,mhe. Sarah Chiwamba ametoa zawadi ya chakula kwa kaya 90 zinazoishi katika mazingira magumu wilayani Liwale kwa ajili ya sikukuu ya idd el fitri.

Akikabidhi zawadi hiyo siku ya  jumamosi juni 24, 2017 alisema kuwa msaada alioutoa ni  mchele kilo 270,maharage kilo 90 pamoja na mafuta lita 90  kwa kaya 90.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ametoa zawadi hiyo baada ya kuguswa na kaya hizo zinazoishi katika mazingira magumu na kuziunga mkono ili kuweza kusherekea sikukuu ya iddi kama familia zingine zinazojiweza. kwa picha zaidi bofya >>HAPA 

Chanzo. (Picha na www.liwaledc.go.tz)

Post a Comment

 
Top