Rais
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L.
Thorton Ikulu jijini Dar es salaam. Katika mkutano huo, uliohudhuriwa
pia na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Balozi
wa Canada hapa nchini, Ian Myles umemalizika kwa mafanikio makubwa
ambapo pande zote zimekubaliana kukaa meza moja kutafuta ufumbuzi wa
changamoto mbalimbali katika sekta ya madini. Habari kamili yaja punde
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment