Benki ya Dunia inatarajia kutoa dola milioni 50 kama msaada wa dharura nchini Somalia ambayo imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ukame mkali.
Katika kikao chake mjini Kenya, benki za maendeleo zimesema kuwa zimekuwa zikiongeza misaada Somalia kuziba pengo la wafadhili waliojitoa.
Benki ya maendeleo ya Afrika ilisema mwezi uliopita kuwa ingetoa zaidi ya dola bilioni moja kukabiliana na ukame katika bara la Afrika.
Sehemu kadhaa za bara la Afrika zinakumbana na ukame mkali huku zaidi ya watu milioni 26 wakikabiliwa na njaa kali.
Post a Comment