0
Mtu mmoja anayeandamana akibeba bango lililosema ni kwa nini unakerwa ninapokula wakati umefungaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMtu mmoja anayeandamana akibeba bango lililosema ni kwa nini unakerwa ninapokula wakati umefunga
Kundi moja la wanaharakati wa haki za kibinaadamu nchini Tunisia limeshutumu kufungwa jela kwa mtu aliyevuta sigara hadharani wakati wa siku ya Ramadhan.
Mahakama ya kaskazini magharibi mwa mji wa Bizerte ilimuhukumu mtu huyo kifungo cha mwezi mmoja jela kwa kukera watu katika maeneo ya uma.
Uamuzi huo unakiuka uhuru wa kibinafsi wa haki ya kula na kunywa katika maeneo ya uma wakati wa mwezi wa Ramadhan.
Wiki mbili zilizopita, watu wanne walihukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela baada ya kula katika maeneo ya uma.
''Hakuna sheria katika taifa hilo la kiislamu zinazomtaka mtu kufunga ama kuwazuia kula ama kuvuta sigara hadharani wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan'', kulingana na Amnesty.
''Mamlaka ya Tunisia haifai kuruhusu mashtaka yasiokuwa na msingi kutumika kuwahukumu raia'' ,iliongezea.''Kila mtu anafaa kuwa na haki kufuata imani zao kuhusiana na maswala ya kidini na maadili''.
Tunisia inajulikana kuwa taifa huru la Kiislamu duniani na lina umaarufu na watalii wengi kutokana fukwe zake za bahari.
Hatahivyo idadi kubwa ya raia ni Waislamu wahafidhina na wanaunga mkono sheria za Kiislamu.

Post a Comment

 
Top