0
María Lorena RamírezHaki miliki ya pichaFOTOGRAFIX
Image captionMaría Lorena Ramírez akiwa jukwaani baada ya ushindi
Mwanamke wa miaka 22 kutoka jamii ya kiasili Tarahumara nchini Mexico ameshinda mbio za kilomita 50 akiwa amevalia ndala.
María Lorena Ramírez aliwashinda wakimbiaji wengine 500 kutoka mataifa 12 katika kitengo cha wanawake huko Puebla, Mexico ya kati.
Hakuvaa mavazi yoyote ya kukimbia, na ndala zake inaarifiwa zimetengenezwa kutoka raba ya matairi yalioharibika.
Jamii ya Tarahumara inasifika sana kwa kuwa wakimbiaji mahiri.
Mbio hizo zimefanyika Aprili 29 lakini habari kuhusu ushindi wake zimechipuka hivi punde.
Kando na kwamba alivalia ndala lakini pia alivalia sketi na kitambaa shingoni kukimbia katika mbio hizo. Hakupokea mafunzo yoyote ya kukimbia.
Alishinda kwa kukimbia kwa kasi ya saa saba na dakika tatu, na alituzwa pesos 6000 ambazo ni sawa na dola 320
Taarifa zinasema kazi yake ni kuchunga ng'ombe na mbuzi na hutembea kati ya kilomita 10- 15 kwa siku.
Mwaka jana aliibuka wa pili katika mashindano ya kilomita 100 yaliofanyika huko Chihuahua.

Post a Comment

 
Top