0
Image may contain: house and outdoor
      Ofisi ya mtendaji wa vijiji cha Mbaya katika kata ya Mbaya wilayani Liwale.


Mkutano cha chama cha ushirika cha NAMBANA uliofanyika leo mei 23 katika kijiji cha Mbaya wilaya ya Liwale mkoani Lindi umevunjika huku baadhi ya wanachama zaidi ya 90 wakijiondoa kutokana na chama hicho kushindwa kuwalipa pesa baadhi ya wakulima.

Diru za habari zinaeleza kuwa mkutano huo ulivunjika mara baada ya kusomewa mapato na matunzi huku mapato yakiwa madogo na matumizi kuwa makubwa zaidi.

Hata hivyo wagombea waliomba nafasi mbalimbali katika chama hiko walikuwa 5 tu huku wanachama wakiwa na hofu kuwania nafasi za uongozi kutokana na chama hicho kufanya vibaya simu wa mwaka 2017.

Chama cha ushirika cha NAMBANA kimeundwa kwa kujuisha jumla ya vijiji 3 ambavyo ni Namihu,Mbaya na Namtumbwa.

Post a Comment

 
Top