
Ahmad Mmow, Lindi.
Mwenge wa Uhuru ambao umeanza kukimbizwa leo katika mkoa wa Lindi, unatarajiwa kufungua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi miradi 51 yenye thamani ya shilingi 11.240.016.805/= iliyopo katika halmashari sita zilipo katika mkoa huu.
Hayo yameelezwa leo katika kijiji cha Litipu wilaya Lindi na mkuu wa mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi alipokuwa anapokea mwenge huo kutoka kwa mkuu wa Mtwara, Halima Dendego. Zambi alisema mafanikio yamiradi hiyo yamefikiwa kutokana na ushirikiano uliopo baina ya serikali, wananchi na washirika wamaendeleo.
Mkuu huyo wa mkoa alibainisha kuwa miradi hiyo yenye thamani ya shilingi 1.37 bilioni imetokana na nguvu za wananchi, halmashauri shilingi 771.51 milioni, Serikali kuu 5.75 bilioni na wahisani 3.33 bilioni.
“Kwakuzingatia ujumbe wa mwenge wa Uhuru mwaka huu 2017, usemao shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu. Nikuhakikishie (kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa) kuwa sisi viongozi na wananchi tumejipanga na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hiyo,” alisema Zambi.
Katika kufikia azma ya utekelezaji wa kauli mbiu hiyo kwa vitendo, Zambi alisema wameanza kuyatambua maeneo, kuyapima na kuyatenga kwa ajili ya shuguli za uwekezaji. Huku wakiendelea kuwahamasisha wadau, wananchi na taasisi mbalibali kuja kuwekeza katika mkoa huu ili kuibua fursa za viwanda vidogovidogo.
Aidha Zambi alieleza kuwa mkoa huu umeendelea kusimamia na kutekeleza kampeni mbalimbali za kitaifa. Ikiwamo mapambano dhidi ya rushwa, dawa za kulevya, malaria na UKIMWI.
Alizitaja hatua zilichokuliwa ilikufanikisha mapambano hayo kuwa ni kuwashirikisha na kuwapa elimu kuhusu madhara ya ngono zisizo salama, kutozingatia usafi, madawa ya kulevya na rushwa.
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika wilaya zote tano za Liwale, Lindi, Ruangwa, Kilwa na Nachingwea. Ambazo zinaunda mkoa huu wa Lindi, nakukimbizwa kilometa 1,202.
Post a Comment