0


Mbunge wa Jimbo la Liwale,mhe. Zuberi Kuchauka ameitaka serikali kuhakikisha inajenga ghala la chakula katika mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na kuimarisha zao la ufuta.

Mbunge huyo amewashauri wasomi  nchini kuwa na utaratibu wa kusoma jiografia ya nchi ili kuwawezesha kufahamu utofauti wa huduma zinazozingatia kipindi husika.

Akichangia bajeti ya wizara ya kilimo,mifugona uvuvi mwishoni mwa wiki bungeni Dodoma alisema mikoa hiyo y akusini haina ghala hata moja.

Alisema umefika wakati serikali ikawajengea ghala hata moja wakazi wa mikoa hiyo ya kusini  huku akieleza kwamba mwaka jana wakazi wa Lindi na Mtwara mazao yao yariharibika baada ya mvua kunyesha na kukosa pa kuyahifadhi.


Kuchauka alisema umefika wakati serikali ikalitazama kwa umakini zao la ufuta kwa kulitengenezea bodi yake na kuiondoa kwenye mazao mchanganyiko,jambo litakaloleta tija kwa wakulima wa zao hilo.

Post a Comment

 
Top