0

Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Katika kufikia na kufanikiwa mpango wa serikali wa kuwa na nchi yenye uchumi wa viwanda. Wakulima wilayani Lindi wameaswa kushiriki utekelezaji wa dhamira hiyo.
Wito huo umetolewa  kijijini Kiwalala, na mmoja wa wakikimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa, Frederick Ndahani, alipozungumza na wananchi kwa niaba ya kiongozi za mbio za mwenge wa uhuru kitaifa. Ndahani alisema wakulima wanawajibu wa kushiriki kikamilifu wa kuifanya nchi kuwa na uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo.
Alibainisha kwamba idadi kubwa ya wananchi wanaoishi wilayani humo ni wakulima, hivyo wananafasi ya kushiriki mpango huo wa serikali kupitia kazi wanayofanya. Ndahani alilifanua kuwa ili wakulima waweze kufanisha azima hiyo hawanabudi kubadilisha mtazamo na fikra kutoka kwenye kilimo cha kawaida na kwenda kwenye viwanda.
“Badala ya kuuza mazao ghafi wakulima wafikirie kuuza yaliyotengenezwa viwandani. Kwakufanya hivyo mtakuwa mmeongeza thamani mazao mnayozalisha,” alisema Ndahani.
Aliongeza kuzitaja faida za kuwa na nchi ya viwanda kuwa ni kuongeza ajira ya mtu mmojammoja, kukuza uchumi wa taifa na kutoa fursa zinazo toa ajira.
“Lengo nikuona hadi kufikia mwaka 2025 wananchi wameondoka kwenye lindi la umasikini nakufikia uchumi wa kati,” alisisitiza Ndahani.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika siku yake ya kwanza kukimbizwa mkoani humu, utalala katika kijiji na kata ya Kiwalala, tarafa ya Mtama wilaya ya Lindi.

Post a Comment

 
Top