
Ilikuwa jumatatu ya tarehe 22 April 2017 katika mji wa Auckland nchini New Zealand, Dunia ilishuhudia mwanariadha mwenye umri wa miaka 101 Man Kaur, aliyeweza kushinda mbio za mita 100 wakati wa mbio za World Masters Games mjini humo Auckland, ambapo pia aliweza kusherekea ushindi wake kwa kucheza densi kidogo. Bi Kaur alimaliza mbio hizo kwa muda wa dakika moja na sekunde 14 na ndiye aliyekuwa mwanariadha pekee kumaliza mbio hizo katika kitengo chake.
Vyombo vingi vya habari vya nchini New Zealand na asilimia kubwa ya vyombo vingi vya habari duniani kote vimeweza kulitaja tukio hilo la ushindi wa Bi Kaur kama “muujiza kutoka Chandigarh.” Kaur aliruhusiwa kukimbia baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na kuonekana yupo fiti kwa ajili ya kuweza kushindana katika mashindano hayo ya watu wenye umri mkubwa, na zaidi sana yeye akiwa mwenye umri mkubwa kuliko wengine kwenye kitengo chake. Baada ya ushindi wake Bi Kaur aliweza kuhojiwa na kusema kuwa, “I’m going to run again, I’m not going to give up.” (Nitakwenda kukimbia kwa mara nyingine tena, sitokata tamaa).
Siku kadhaa baada ya ushindi wa Bi Kaur kusikika zaidi na kushinda medali ya dhahabu, mwanae Gurdev Singh aliweza kufanya mahojiano na chombo cha habari cha CNN na kuelezea namna gani mama yake alivyoweza kufikia ndoto yake. Gurdev anasema kuwa mama yake alianza kujifunza kukimbia mbio akiwa na umri wa miaka 93 wakiwa pamoja, na yeye yaani Gurdev ndiye aliyeweza kumshawishi mama yake kufanya hivyo baada ya kuvutiwa na mashindano ya watu wenye umri kama wake na kuamini kuwa mama yake pia anaweza kushiriki na kuwa mshindi.
“Be strong, be fearless, be beautiful. And believe that anything is possible when you have the right people there to support you.” -Misty Copeland

Gurdev anaendelea kusema leo mama yake ameweza kutimiza ndoto yake kwa kushinda medali ya dhahabu kwa mara nyingine tena akiwa na umri mkubwa, na hii ikiwa ni mara yake ya 20 kupata medali za dhahabu katika mashindano mbalimbali ya aina hiyo. Leo Bi Kaur mwenye watoto watatu, wajukuu 10 na vitukuu 12 ameweza kutimiza ndoto yake ya kushinda medali nyingi za dhahabu akiwa na umri mkubwa, hii ni wazi kila kitu kinawezekana. Aliporudi nchini mwake India aliweza kuongea na jamii ya watu wake na kuwaambia maneno haya yenye nguvu, “everyone should do this” (kila mmoja lazima anaweza kufanya hili). Hakika naamini hata mimi na wewe tunaweza kufanya hili, kama Bibi mwenye umri wa miaka 101 ameweza kushinda medali nyingi za dhahabu itakuwaje mimi na wewe kushindwa kutimiza ndoto zetu tulizonazo?
Mara nyingi tunajikuta tunakata tamaa kwenye kutimiza ndoto zetu na hata kusingizia mambo mbalimbali kama vile elimu ndogo, umri wangu mkubwa au mdogo kutimiza jambo hili, sina kipaji chochote cha kunisaidia kutimiza ndoto yangu, sina mtaji wa kutosha kujiajiri na mengine mengi tunayoyatumia kama “excuses” ya kutokuamua kwa makini kuchukua hatua na kufanikiwa. Hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa kwa kuogopa kuchukua hatua zenye kuleta matokeo makubwa kwenye maisha yake. Huwezi kufanikiwa kwa “kujihurumia,” wakati mwingine ni lazima ujitoe haswaa kwenye kutimiza ndoto zako maadam umri wako unaruhusu kufanya jambo lolote unalotaka, amua kulifanya kwa bidii hadi uone matokeo makubwa juu yake.
Jambo lingine unalolihitaji kulitambua katika maisha yako ni kumpata mtu anayeweza kukusaidia kuamini katika uwezo mkubwa ulionao. Bi Kaur kabla ya kuwa mwanamichezo anayejulikana sana leo na kushinda medali karibu 20 katika umri wake mkubwa, hakuwahi kujulikana hapo kabla hadi alipotimiza miaka 93 na mtoto wake Gurdev kuona uwezo mkubwa alionao mama yake, ndipo alipoamua kumfundisha (training) kukimbia hadi alipofanikiwa kuwa mshindi wa medali ya dhahabu kwenye mashindano makubwa ya World Masters Games.
Faith makes all things possible… love makes all things easy. -Dwight L. Moody
Jiulize leo ni nani anayeamini uwezo ulionao, ni mtu gani amekuwa akikusisitiza mara kwa mara kushikilia jambo fulani unalolifanya hadi uone matokeo, ni watu wangapi uliowahi kukutana nao wanaokuambia juu ya uwezo mkubwa ulionao kwenye maisha yako na eneo fulani? Amua leo kuwa karibu na watu wanaoamini katika kile ulichonacho ndani yako na uwe na utayari wa kuwasikiliza ili wakupatie mawazo mazuri yanayoweza kukusaidia kutimiza ndoto zako. Kumbuka ndoto yako inawezekana. Kila wakati, kila dakika na kila muda jiambie binafsi moyoni mwako ndoto yangu inawezekana.
Post a Comment