Wayazidi 36 walipelekwa Dohuk Kaskazini mwa Iraq
Ofisi ya Umoja wa
Mataifa nchini Iraq, inasema kuwa watu 36 wa kabila la Yazidi,
waliotekwa kama watumwa na kundi la Islamic State, wameokolewa wakiwemo
wanawake na watoto.
Wanaripotiwa kuwa kizuizini kwa karibu miaka mitatu.Islamic State iliwauwa na kuwateka watu wengi wa Yazidi, ambao ni wa dini tofauti, wakati IS iliteka eneo la kaskazini mwa Iraq, mwaka 2014.
Wakurdi wa Peshmerga walidhibiti eneo hilo mwaka 2015 lakini Wayazidi wengi walikiliwa na Islamic State maeneo mengine wakati kundi hilo lilidhibiti sehemu kubwa za Kaskazini mwa Iraq.
- Wanawake wa Yazidi washinda tuzo ya Sakharov
- IS yalipiza kisasi harusini Iraq
- Majeshi ya Iraq yashambulia IS
Wanajumuishwa na familia zao huko na kupewa mahitaji ikiwemo nguo na madawa pamoja na ushauri wa kisaikolojia.
Umoja wa mataifa unaamini kuwa hadi wanawake na wasichana 1500 bado wanashikiliwa na huenda wanakumbwa na dhuluma za kingono.
Post a Comment