0
Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinafanyika leo April 26, 2017 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa zaidi ya watumishi elifu tatu tayari wameshahamia Dodoma, ambapo awamu ya pili na ya tatu ya kuhamia dodoma imepangwa kutekelezwa mwaka ujao wa fedha na serikali imetenga takribani ya shilingi bilioni mia mbili kwaajili ya kujenga ofisi na nyumba za viongozi wa serikali.

" Mimi na Dkt.Shein tutaulinda muungano kwa nguvu zote, na kamwe asijitokeze wa kuuvunja muungano atavunjika yeye." alisema Rais Magufuli

Ameyazungumza hayo wakati wa maadhimisho ya sherehe za muungano wa miaka 53 ya Tanganyika na Zanzibar, Makao makuu ya nchi Dodoma.

Post a Comment

 
Top