Dodoma. Mwenyekiti wa Taifa CCM, Rais John Magufuli amewataka
makatibu wa mikoa wa chama hicho wanaotaka kuingia katika vikao vya
Halmashauri Kuu (Nec) ya Taifa ya chama hicho wakagombee uenyekiti.
Akizungumza leo (Jumamosi) wakati wa ufunguzi wa kikao cha Nec, Rais Magufuli amesema
kuna watu wanaumuhimu wa kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu na
kwamba wakikosa kutakosekana uwakilishi .
“Nikawaambia mbona mwaka uliopita waliposimama wakimpinga mwenyekiti
makatibu mlikuwepo? Wakati mwenyekiti anawalipa mshahara mbona
hamkumtetea? Mbona hamkusimama kupigana na bado wakaendelea kuimba
wanaimani na mtu fulani na wengine mkawa mnaitikia,”amesema.
Amesema kwa kuwa mabadiliko ya Katiba na Kanuni ambayo yatapunguza
idadi ya wajumbe wa vikao vya juu vya chama hicho walishayajadili
katika kikao kilichofanyika Desemba 13 mwaka jana, ni matumaini yake
kuwa kikao hicho hakitachukua muda mrefu kuyajadili.Mwananchi
Recent Posts
- KARIBU MWENGE WA UHURU 2022 WILAYANI LIWALE APRIL 29,202223 Apr 20220
Wasaanii mbali mbali watakuwepo kukesha nasi! Msagasumu, Dr nyau wakishirikiana na wasanii wa ndaniRead more »
- WATANZANIA TUSIKUBALI KUCHONGANISHWA-MAJALIWA10 Jun 20181
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasikubali kuchonganishwa na kwamba Serikali haiongozwi kwa misingi ya kidini bali imeziachia ta...Read more »
- Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 09.06.201809 Jun 20180
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionAliyekuwa beki wa zamani wa klabu ya Real Madrid fernando Hierro Aliyekuwa beki wa Real Madrid Fernando ...Read more »
- WANANCHI WA KIGOMBE WATAKIWA KUACHANA NA BIASHARA ZA MAGENDO09 Jun 20180
MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kigom...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.